Hofu ya  Virusi vya  Corona  yazuia  ulevi Murang’a

WA IRIA
WA IRIA
Gavana  wa Murang’a  Mwangi wa Iria amefutilia mbali leseni za  wamiliki wa mabaa waliokaidi  agizo la kuyafunga maeneo hayo ya burudani  kama ilivyoagizwa na  kundi la kushughulikia dhrura katika kaunti hiyo .

Siku ya jumatatu  gavana huyo na kamishna wa kaunti Mohamed Barre  walisema  mrundiko wa watu  na hali mbaya ya usafi huenda ikalazimu kufungwa kwa baadhi ya baa .waliwashauri wakaazi kuburudi kwa kwa vinywaji vyao wakiwa nyumbani .

Wawili hao walisema watu walevi hawataweza kujikinga dhidi ya virusi vya corona .Kufikia jumanne gavana wa Iria alisema leseni za baa hio zimefutiliwa mbali baada ya wenyewe kukosa kuafikia mahitaji yaliyotolewa kama mojawapo ya njia za kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona .