Hofu yatanda Likoni feri, simu yawaka moto ndani ya MV Harambee

unnamed (4)
unnamed (4)
Raia wameshtuka ghafla baada ya simu ya jamaa mmoja kulipuka na kuwaka moto katika feri ya MV Harambee.

Tukio hili limejiri wakati jamaa huyo alijaribu kutoa simu kwenye mkoba wake.

Jombi huyo hakusita na mara ghafla akaitupa simu bahari Hindi

"Polisi wanachunguza kisa hiki kilichofanyika saa tatu asubuhi..." Shirika la feri lilichapisha Twitter.

Zaidi wa watu takriban laki 300 na magari 6,000 hupitia katika kivukio hicho kila siku.

"Saa tatu asubuhi, simu ya abiria wa kiume imelipuka na kutoa miale ya moto akijaribu kutoa mkoba wake..." ilichapisha shirika hilo.\

https://twitter.com/FerryKenya/status/1189093314517241856

Eneo hilo la Likoni limetajwa kama sio salama kwa maisha ya wanaovuka baada ya kusababisha kifo cha Mariam Kighenda na Amanda.

Utepetevu wa wafanyakazi feri umetuhumiwa kama sababu kuu ya ajali katika kivukio hicho cha bara Hindi.

Operesheni zilianza Likoni feri mwaka wa 1937.