Kila siku wanayoripoti kazini kuwahudumia wagonjwa ni hatua moja wanayojitia karibu na uwezekano wa kuambukizwa ugonjwa huo. Ripoti zaarifu kwamba wahuduu wa afya, maafisa wa kliniki na wauguzi wameambukizwa ugonjwa huo na hata wengine wameaga dunia.
Kifo cha wiki jana cha daktari Doreen Lugaliki ni ishara tosha kwamba wahudumu hao wa afya wapo katika hatari zaidi kuliko kitengo chochote cha wapambanaji dhidi ya janga la corona.
Serikali na wadau wengine wamejaribu kuwapa hakikisho la usalama wao wa kutoa vifaa kama vile PPE lakini misaada hiyo haijatosha jambo ambalo linazidi kuhatarisha maisha ya wahudumu wengi.
Licha ya hatari hiyo wahudumu wengi wa afya wamejitolea muhanga kuendelea na kazi zao na mengi yanafaa kufanywa ili kuwalinda kwani wao pia wana familia na wapendwa wao watakaoathirika sana endapo wataangamia katika janga hili la corona.