bhang-768x461

Holy Herb:Ajuza mwenye umri wa miaka 83 akamatwa na Bangi Nyeri

Ajuza  mmoja mwenye umri wa miaka 83  aliyepatikana na gramu 600 za bangi  amekiri  mashtaka ya kuwa na bangi katika mahakama ya Nyeri . Lydia  Mumbi  alikamatwa na bangi hiyo yenye thamani ya shilingi  500 katika eneo la Mthinga ,Tetu .  Bikizee huyo atasalia katika seli hadi jumatatu wakati  atakapofikishwa tena kortini baada ya maelezo zaidi kuhusu kesi yake kufahamika .

Mbunge akamatwa na maafisa wa EACC.

Kwingineko polisi huko kakamega wamewakamata wanafunzi 19  waliopatikana na misokoto kadhaa ya bangi  na pombe haramu . kamanda wa polisi wa  kaunti ndogo ya muamis mashariki Joseph Ongaya  amethibitisha kukamatwa kwa wanafunzi hao wa shule ya upili ya Mwitoti . Mwalimu mkuu wa shule hiyo ndiye aliywafahamisha polisi ,ambao walifaulu kuwakamata wanafunzi 19  ambao walihojiwa kwa siku mbili na makachero kuhusu tukio hilo . mabunda kadhaa ya miraa na sacheti zenye pombe haramu pia vilipatikana kutoka kwa wanafunzi hao .

Unyama:Mwanamke awaua wanawe wawili Nandi

Gavana wa kaunti hiyo  Wycliffe Oparanya  awali alikuwa amehusisha ongezeko la matumizi ya mihadarati na kuongezeka kwa visa vya uhalifu  pamoja na biashara haramu ya uuzaji wa pombe haramu kwa wanafunzi wa shule za kaunti hiyo .

 

 

Photo Credits: radio jambo

Read More:

Comments

comments