HONGERA!! Bien wa Sauti Sol afunga ndoa na mpenzi wake Chiki

Baada ya mda mrefu wa kungoja, msanii wa bendi ya Sauti Sol, Bien Barasa mwishowe amefunga ndoa na mpenzi wake wa zamani Chiki Kuruka.

Wawili hao walifunga ndoa katika mtaa wa Lavington, Nairobi hii leo katika hafla ambayo ilikuwa ya walioalikwa pekee katika mkahawa mmoja karibu na barabara ya James Gichuru.

Mwandani wetu alituambia kuwa hafla hiyo ilikuwa imefanywa siri kuu huku jamaa marafiki na ma celeb wakiwa miongoni mwa walioalikwa.

Hafla hii ina mitindo ya zama za kale.

Hapo awali, Bien alikuwa tayari kufanya harusi ya kitamaduni baada ya kusema kuwa harusi ya kisasa almaarufu 'white wedding' ni kama 'ukoloni'

Cha kushangaza ni kuwa wageni walipewa mwaliko siku moja kabla ya siku kuu na walishauriwa kuwa wameketi kabla ya saa nne unusu asububu.

Pia walishauriwa kuwasili humo na teksi na sio kwa gari zao kwani kungekuwa na shida ya kuegeza magari.

Wawili hao walisema kuwa waliahirisha harusi yao mwaka uliopita kwa sababu wazazi wa Chiki hawakuwa nchini.

Mipango ya harusi iliwekwa chini ya maji kwani hawakutaka wanahabari wajue. Mwandani wetu alitueleza kuwa wawili hawa walitumia mamilioni ya pesa kuandaa harusi hiyo.

“The wedding is at Lavington right and only few celebs are invited. It is a very secret event with tight security. No gate crashers or media”

Tunawatakia wapenzi hawa wawili kila la heri katika ndoa yao.