Hongera kwa kazi nzuri ,Diamond asema

pjimage (11) (1)
pjimage (11) (1)

NA NICKSON TOSI

Diamond aliandika ujumbe wa kumhongera Harmonize baada ya kutoa albamu yake ya kwanza mwaka huu 2020.

Wikendi Harmonize alizindua alibamu hiyo kwa jina AFROEAST katika tamasha iliyoudhuriwa na rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kama mgeni mkuu.

Masaa tu baada ya kuzinduliwa ,Diamond aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akimshukuru kwa kazi nzuri na kuwarai wafwasi wake kuiendeleza kazi hiyo ya Harmonize.

Hakikisha kuwa unajinyakulia na kufahamisha wengine kuhusiana na  albumu mpya ya Haromonize,inapatikana katika mitandao yote.aliandika Diamond.

Ujumbe huo uliwavutia mashabiki zaidi ya alfu 20000 waliotuma jumbeza kumsifia Harmonize .

Licha ya Harmonize kukosa kumwalika msanii hata mmoja kutoka kwa lebo ya WCW ,wengi walishangazwa na hatua ya Diamond ya kuwaomba mashabiki kuisikiliza kazi hiyo mpya kutoka kwa Harmonize.

Konde Boy katika albamu hiyo aliyoizindua eneo la Milimani ilikuwa na nyimbo 18 ambazo zote aliziimba wakati wa uzinduzi wake.

Katika albamu hiyo,wasanii kama Morgan Heritage,Khaligraph jones,Mr Blue,Lady Jaydee,Phyno,Dj Seven,Yemi Alade ,Mr Eazi Falz na Burna Boy wote wameshirikishwa.
Wageni wengine waliohudhuria hafla hiyo ni kama Ommy Dimpoz,Darasa,Mr Blue,Hamisa Mobetto,Coutry Boy,Mario na wengine wengi.