Hongereni! Sauti sol wazindua albamu yao mpya ya 'Midnight Train'

Bendi ya Sauti Sol hatimaye wametoa albamu yao ya tano, albamu hiyo inafahamika kama 'midnight train' ni albamu ambayo ina vibao kumi na tatu, vibao hivyo vinaangazia hofu ambayo watu wengi hupitia katika maisha yao, majaribio na hata changamoto.

Kibao Midnight train kimezalishwa na Andre Harris (Justin Bieber, Kanye West, Jill Scott) kinazungumzia bidii yao ambayo wameweka katika kazi yao ya usanii, na hata kuweka blanketi kando na kisha kufanya kazi bila kusinzia.

"WE’VE HAD AN AMAZING JOURNEY SO FAR AND IT’S LIKE AN EVER MOVING TRAIN. EACH TIME WE MAKE IT TO A DESTINATION WE REALIZE THE ROAD DOESN’T STOP THERE. WE CONTINUE TO BETTER OURSELVES AND LOOK FORWARD TO BRINGING OUR FANS ALONG WITH US AS WE GROW." Alizungumza Chimano.

Awali bendi hiyo ilitoa kibao cha 'suzanna' ambacho kilipendwa na wengi. Baada ya hapo walitoa 'insecure ambayo kwa sasa inafanya vyema kwenye mitandao ya kijamii.

Katika albamu yao kuna kibao ambacho kinafahamika kama 'Disco Matanga' ambacho wamemshirikisha msanii Sho Madjozi, kama vile walivyosema kwa hakika wasanii au bendi hiyo wametia bidii kwa kazi yao.

Hivi hapa vibao ambavyo viko katika albamu hiyo;

1. Intro

2. Midnight Train

3. Insecure

4. Feel My Love

5. Brighter Days ft. Soweto Gospel Choir

6. Nenda Lote

7. Suzanna

8. Set Me Free (Interlude)

9. My Everything ft. India Arie

10. Wake Up ft. Mortimer

11. Sober

12. Rhumba Japani ft. Kaskazini, Bensoul, Xenia, Nviiri the Storyteller, Okello Max, NHP

13. Disco Matanga (Yambakhana) ft. Black Motion & Sho Madjozi