Huddah ananini cha kunitosheleza mimi? Adai Khaligraph Jones

Cheche za maneno zimeanza kushuhudiwa katika mitandao ya kijamii  baina ya Khaligraph Jones na mwanasosholaiti Huddah Monroe baada ya Huddah kudai kuwa hajui iwapo kuna msanii nchini Kenya kwa jina Khaligraph na hajui hata wimbo wowote wa msanii huyo.

Kulingana na Huddah alikuwa anapokea simu mara nyingi kutoka kwa mtu asiyemfahamu na hakushika simu hiyo kwa kile alisema huwa hapendi kushika simu za watu ambao hawajui.

Kama njia ya kujibu madai ya Huddah, Papa Jones alikubali kuwa alimpigia wakati mmoja simu kichuna huyo japo hakushika .

“Huddah simu hashiki anadhani nataka kumpiga miti. Nina wife joh sipendi hizo kiki, na nimewachana na huyo mjinga” alisema Khaligraph Jones

Akizungumza na rafiki wa karibu Huddah alidai kuwa hana ufahamu iwapo kuna msanii nchini ambaye anajulikana kama Jones na hata baada ya kusoma yale Papa Jones alikuwa ameandika kuhusiana na yeye haikumhusul ndewe wala sikio .

Huddah vile alionmgeza kuwa na usemi huo aliokuwa ameandika Papa Jones kuhusiana na yeye ,ilimfanaya kuenda katika mitandao yake kudhibitisha kama ni yeye.

Aliongeza kuwa licha ya kutokuwa na ufahamu wowote wa nyimbo zake alikuwa anafanya vizuri kufwatia picha za tuzo alizoziona katika ukurasa wa Papa jones.

'Jamaa alinipigia simu mara nyingi sana na sikushika simu hiyo kwa kuwa mimi huwa sishiki simu,kwa kweli mimi sifahamu nyimbno zozxote za Khaligraph jones lakini nadhani anafanya vyema na pia ameshinda tuzo ,mbele ya Mungu leo ndio mimi nimeangalia mitandao yake''álisema Huddah

 
Huddah aidha kama njia ya kumdhihaki Papa Jones alisema kuwa anawafahamu tu Nyashinski na Octoppizo kama wasanii wa kufoka/rapper nchini ambao wanafanya vyema  ikilinganisha na wasanii wengine.
Nawajua Octoppizo na Nyashinski kutoka Kenya ambao wanafanya vizuri kimuziki na mimi napenda nyimbo zao sana ikilinganishwa na wasanii wengine,alisema Huddah