Huduma za kaunti kulemazwa kuanzia kesho

Huduma za serikali za kaunti zitalemazwa kuanzia kesho  baada ya  maseneta kukosa kupitisha mswada wa mfumo unaofaa kutumiwa kwa ugavi wa mapato .

kUpitia taarifa ,mwenyekiti wa baraza la magavana Wycliffe Oparanya  amesema vituo vya afya havitawachukua wagonjwa wapya na vitakuwa vikitoa huduma adimu kwa wagonjwa wa kutibiwa na kurejea nyumbani

Oparanya  amesema huduma zote zisizo za msingi zimesitishwa mara moja na wafanyikazi wa kaunti wameshauriwa kuchukua likizo ya wiki mbili

Amesema katika taarifa hiyo kwamba serikali za kaunti zitazidi kuishinikiza serikali kuu kutoa pesa za kaunti .

Oparanya  amesema wafanyikazi wa kaunti wakiwemo wahudumu wa afya hawajalipwa kwa miezi mitatu .Ameongeza kwamba  serikali zote 47 za kaunti zinapitia  uchungu kwa ajili ya ukosefu wa fedha na suluhisho ni kwa hazina ya kitaifa kutoa fedha .

Senate kwa mara ya kumi ilishindwa kupata mwafaka kuhusu jinsi fedha zinavyofaa kugawanywa kwa kaunti .Hii ni licha ya rais Uhuru Kenyatta kuahidi kuzipa kaunti shilingi bilioni 50 za ziada katika mgao wa bajeti ya mwaka ujao wa kifedha .