Huduma za treni kutoka Nairobi zasimamishwa kuanzia leo hadi Januari 6

reli
reli
Shirika la Reli nchini limesimamisha huduma za treni kutoka Nairobi kuanzia leo hadi Januari 6. Kaimu meneja wa masuala ya Kibiashara Margaret Kawira anasema huduma hizo zimesitishwa kwa sababu ya kupungua kwa idadi ya wasafiri.

Treni hizo hutumika kuelekea Ruiru, Embakasi, Kikuyu na Syokimau.

Mkusanyiko wa habari;

Kama mzazi unashauriwa kupunguza muda ambao mwanao anatumia mtandaoni na unafaa kufahamu tovuti anazotembelea.

Mtaalam wa usalama wa mitandaoni Byron Adera anasema kuwa mfahamivu wa kile wananchofanya mtandaoni kutakusaidia kuwaongoza.

Kuwa na wasiwasi kama mzazi ikiwa mtoto wako atakuficha siri zake. Mwanasaikolojia Riziki Ahmed anashauri uanzishe uhusiano wazi wa mawasiliano na mwanao ili aweze kukuona kama mtu wa kumuongoza na wala sio mtu wa kumhukumu.

Hakikisha unamwona daktari iwapo umekuwa ukiendesha na kutapika kwa zaidi ya masaa 24 kwani huenda ukawa unaugua sumu ya chakula. Daktari Anthony Akoto anasema hali hii inaweza kuwa hatarai sana kiafya hususan ikiwa una hali ya kiafya kama ugonjwa wa kisukari.

Kama mteja una haki ya kuchagua kiti chako katika gari za usafiri wa umma. Simon Kimutai kutoka muungano wa wamiliki wa Matatu anasema kuchagua kiti ambacho uko sawa nacho ni muhimu haswa unapoenda safari za mbali.

Iwapo wewe hutumia barabara ya mbagathi unashauriwa kutumia njia mbadala kuanzia tarehe 27 mwezi huu kwani barabara hiyo itakuwa imefungwa. Mamlaka ya barabara za mjini KURA inasema barabara hiyo itafungwa ili kupa nafasi kwa ujenzi wa kivuko cha kisasa.