Huenda Kitaumana! Vita dhidi ya virusi vya Corona huenda vikasababisha matatizo zaidi

mATATU
mATATU
Iwapo ulifikiri kwamba vita dhidi ya virusi vya Corona havitakufikia na kuathiri maisha yako ya kawaida ,basi funga mshipi kwa sababu msukosuko unaokuja endapo hatutathibiti  virusi hivyo  katika wiki moja ijayo .

Serikali imetangaza mikakati na hatua mbali mbali katika jitihada za kuthibiti maambukizi ya virusi hiyvo.Baadhi ya hatua hizo huenda zikawavuruga wengi kiuchumi na jinsi wanavyoendesha maisha yao

1.Usafiri wa PSV

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema matatu hazifi kuwabeba abiria kujaa katika magari yao. Matatu za abiria 14 kwa mfano zimetakiwa kuwabeba abiria wanane .endapo hawatofidiwa kwa viti vitakavyosalia bure ,huenda wahudumu wa matatu wakaipisha gharama hiyo kwa wasafiri . itakugharimu zaidi kusafiri kutoka sehemum oja hadi nyingine au hata  unapokwebda kazini .

Iwapo hali hiyo itasalia jinsi ilivyo sekta ya matatu itapata hasara na kulazimika kusitisha au kulemaza oparesheni zake .watakaoathiriwa sana ni wanaofanya kazi katika sekta hiyo ambao sasa watalazimika kurejea nyumbani kwa ajili ya ukosefu wa kazi .wenye magari walio na mikopo na pia watashindwa kulipa mikopo yao kwa sababu ya ukosefu wa pesa . Huenda pia ikawa vigumu kwa watu kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kama ilivyoagiza serikali ya Uganda .hii ni kwa lengo la kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo kutoka  eneo moja hadi jingine .

 2.Ununuzi wa bidhaa

Serikali imewataka wamiliki wa duka kuu kuhakikisha kwamba idadi ndogo ya wateja wanaruhusiwa katika sehemu hizo za ununuzi wa wakati .Huenda  ikalazimika kutumiwa kwa maafisa wa usalama kutumwa katika maduka ya jumla ili kutekeleza agizo hilo na kusimamia foleni ndefu zitakazoshuhudiwa .Itakuchukua muda mrefu kununua unachotaka na endapo hali haitaboreka huenda hata kiwango cha bidhaa unazotaka kununua kikathibitiwa ili uwaruhusu watu wengine pia wapate bidhaa muhimu kama vyakula na dawa .

 3.Maeno ya Burudani /Baa

Maeneo haya ndio yamepigwa na butwa abaada ya sertikali kutangaza kwamba yanafaa kufungwa kufikia saa moja unusu kila siku .muda huo ndio huwa kilele cha biashara zao na hatuaya kuyataka mabaa kufungwa mapema ni kukaribisha hasara ya mamilioni ya pesa .sekta ya vileo imewaajiri zaidi ya watu robo milioni na agizo hilo linazitia kazi zao katika hatari . Tayaro kaunti 16 zimepiga marufuku kufuguliwa kwa mabaa katika sehemu zao wakati huu wa kukabiliana  na virusi vya Corona.

 4.Kufungwa kwa biashara

Biashara kadhaa zinazohusisha watu wengi katika sehemu moja huenda zikaagizwa kufunga ili kuzuia mrundiko wa watu .tayari baadhi ya kaunti zimepiga marufuku   masoko ya wazi ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona .endapo hilo litafanyika kote basi itakuwa vigumu kusalia majumbani bila chakula kwani masoko yote  yatakuwa yamefungwa. Biasha nyingi ndogondogo pia zitakosa pesa na wateja na hivyo basi kulazimika kufungwa  bila kutaka .

 5.Watoto nyumbani

Kabla ya serikali kutangaza shule zote na taasisi za elimukufungw ,wazazi hawakuwa na bajeti ya kukimu mahitaji ya wanao nyumbani .kwa sasa ,bajeti ya chakula imeongezeka baada ya wanafunzi kuagizwa kurejea nyumbani .iwapo muda wa kusalia nyumbani utazidi ,hali itakuwa ngumu zaidi kwa sababu chakula kinachotegemewa hata sokoni na mashambani kitazidi kupungua kwani hakuna atakayeweza kuendelea na kilimo, mavuno au hata usafairishaji wa chakula hadi katika maeneo ya miji .