Watahiniwa wa KCPE na KCSE huenda wakaifanya mitihani hiyo ya kitaifa Aprili mwaka ujao ,waziri wa elimu George Magoha amesema .
Magoha amesema Aprili ndio muda wa mwisho ambao mitihani hiyo inaweza kufanywa iwapo shule zitafunguliwa mwezi septemba kama ilivyoagizwa na rais Uhuru Kenyatta .
" kuhusu kalenda ya shule ,serikali inafaa kuzingatia muda wa mwisho ambao shule zinavyoweza kufunguliwa na watahiniwa kuifanya mitihani’ amesema Magoha
Magoha amesema majadiliano yanaendelea miongoni mwa wadau na katika wiki mbili zijazo ,itafahamika bayana endapo shule zitafunguliwa septemba ili watahiniwa waweze kuifanya mitihani hiyo kufikia Aprili mwaka ujao
Magoha ameyasema hayo alipofika mbele ya kamati inayoshughulikia hali ya Covid 19 nchini . Kamati hiyo inayoongozwa na seneta wa Nairobi Johnson Sakaja.