Hueng Min Son kuendelea na shughuli za kijeshi - Serikali ya Korea Kusini yasema

NA NICKSON TOSI

Nahodha wa timu ya taifa ya Korea Kusini Hueng Min Son ambaye anachezea klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza ataendelea na shughuli za kijeshi za kulinda taifa hilo baada ya kumaliza siku 14 akiwa amejitenge na wenzake.

Mchezaji huyo wa miaka 27,alirejea katika taifa hilo  Machi 28  mwaka huu baada ya ligi kuu ya Uingereza kusitishwa kwa muda kutokana na Corona.

Kwa mujibu wa sheria za taifa la Korea Kusini wanaume ambao wana maumbile sawa ni sharti wahudumu kwenye vikosi mbali mbali vya kijeshi aghalabu kwa miezi 21.

Son anahudumu kama mwanajeshi wa kikosi cha wanamaji cha Korea Kusini.