HUSSEIN-2-e1572368194979

Hussein Mohamed aiaga Citizen TV, Raila alimbikizia sifa

Kinara wa ODM Raila Odinga ametoa kauli kuhusu uchapakazi wa Hussein Mohamed.

Haya yanajiri huku Hussein akitamatisha kibarua chake katika runinga ya Citizen.

“Alivutia sana kama mtu ambaye anafanya utafiti mzuri wa kazi zake. Anajua majibu ya maswali atakayokuuliza…” Alisema Raila.

Hussein Mohamed aitema runinga ya Citizen, sababu zatajwa

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka alimpongeza kwa kazi nzuri.

Gavana Anne Waiguru, waziri Eugene Wamalwa, mbunge Sabina Chege, mwenyekiti wa chama cha ODM John Mbadi na waziri Farida Karoney walimtakia mema.

Ni bayana kuwa sasa hautoweza kumwona mwanahabari Hussein Mohamed akisoma habari katika kituo cha runinga cha Citizen.

Hapo jana usiku, mwanahabari huyu shupavu ametinga kazi ya miaka mingi katika kituo hiki.

Hussein alikuwa anasoma habari katika kituo hicho pamoja na kufanya mijadala na mahojiano.

Vipindi vyake vilikuwa News Night kila Jumanne na kitengo cha Big Question.

Madini Classic azungumzia Chuchuma ya Willy Paul, sababu za kutoipa shavu

Mohamed amekuwa akisoma habari kwa kipindi cha miaka 10.

Hussein alitangaza taarifa hizi kupitia mtandao wa Twitter siku za hapo nyuma.

Katika kipindi chake cha mwisho hapo jana, Hussein aliwahoji kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Kipchumba Murkomen na kiongozi wa wachache John Mbadi.

Mdahalo huu ulihusu BBI na siasa zinazozunguka mageuzi yanayopendekezwa.

Hussein aliashiria kuwa Oktoba ataacha kazi Citizen kupitia mtandao wa Twitter.

 

“Nimefanya uamuzi kuchukua nafasi ya kumpumzika baada ya Oktoba ili niweze kushughulika na maswala mengine…” Alichapisha Hussein.

Photo Credits: Abraham kivuva

Read More:

Comments

comments