Catherine kamau

Huwa nasikia vibaya watu wakiandika mabaya kuhusu bwanangu na mimi

Catherine Kamau almaarufu Kate Actress alisema kuwa ombi la mtoto wake kuja kuishi na yeye katika nyumba yake ndogo ndio ilimfanya atie bidii katika kazi yake.

Hamstahili kupata hewa ya huru jaji wawaambia wauwaji sita

Katika mahojiano mama wa mtindo mpya alisema kuwa mama yake mzazi aliweza kumsaidia sana kwa kumlea mvulana wake, baada ya kutoka kuishi na mama yake.

Catherine Kamau
Catherine Kamau(Cate Actress)

Licha ya kumfukuza nyumbani walipojua kuwa ana ujauzito.

“Mtoto wangu angenipigia simu akiniuliza ama nimehamia nyumba kubwa ili aje kuishi na mimi,

“Nilianza kuishi katika nyumba ndogo (bedsitter), ningehakikisha kuwa nimeenda kumtembelea mtoto wangu nyumbani mwa mamangu, na mwisho mwa wiki na mchukua nakaa na yeye nyumbani kwangu,” Alieleza Kate.

Mtoto wake alidindia kumsisitizia na kumuuliza kwanini nyumba yake ni ndogo, jambo ambalo ilimfanya apate kutia bidii katika kazi yake.

Paul Pogba to miss second leg of Manchester United’s Champions League

“Kwanini siishi na wewe? angeniuliza, ningelia kila siku na ningeambia Mungu aachejambo hilo liwe motisha yangu,” Kate alizungumza.

Cate actress
Cate mume wake Phil na mtoto wao

Cate kwa sasa ameolewa na Phil Karanja ambao walianza kuigiza pamoja katika kipindi cha Mother-in-law kilichokuwa katika runinga ya Citizen.

“Alikuwa mwelekezi wangu katika kipindi hicho na aliweza nisaidia kukuza kazi yangu, nampenda kwa maana ni mtu mwenye uwezo mwingi,” Aliongea Kate.

Emiliano Sala’s body to be flown to Argentina before a wake on Saturday

Alisema kuwa majibu ambayo anapata mabaya ni akiweka picha yake na mume wake Phil, huku akisema kuwa maisha yake yamekuwa safari na mambo amepitia kisha watu kuandika mambo mabaya kumuhusu.

“Huwa nasikia vibaya watu wakiandika mambo mabaya kuhusu mume wangu na mimi, nikijua maisha yangu yamekuwa ni safari isiyo rahisi,

“Na mambo mengine pia ambayo yanahusiana na mtoto wangu huwa nasikia vibaya sana wakiandika mambo ambayo yanahusu familia yangu,” Catherine alizungumza

 

Photo Credits: file

Read More:

Comments

comments