Huddah-Monroe-1

‘Huwa sishiriki mapenzi na bwana wa wenyewe,’ – Huddah Monroe

Mwanamitindo Huddah Monroe amekuwa akiwekwa katika vitengo mbalimbali na wakenya lakini kama kawaida hayo hayajawahi mpa kiwewe hata siku moja.

Lakini kama kuna kitengo ambacho hupaswi kumweka ni kile cha kuwa yeye hushiriki mapenzi na wanaume waliofunga ndoa. Alisema kuwa hilo sio kombe lake la chai.

Akijulikana kama mmoja wa wanamitindo wakuu zaidi humu nchini, mara kwa mara Huddah alifichua kuwa alipata fedha zake nyingi kupitia kulala na wanaume waliona pochi nene au walio na fedha tele ukipenda. Ila alikana kushiriki mapenzi na wanaume walio katika ndoa.

Kile wengi hudhani ni kuwa wanaume waliokatika ndoa ndio walio na fedha nyingi na ndio maana wengi husema kuwa yeye huwa na tabia ya kuvunja ndoa nyingi.

Lakini ukweli ni kuwa wanaume walio katika ndoa sio kikombe changu cha chai. Yeyote anayenijua anajua kuwa siwezi shirikishwa katika kitengo hicho.


Wiki chache zilizopita alijipata taabani na mama yake baada ya kuwaambia wanawake waache tabia za kukopa pesa kila wakati. Aliwaambia kuwa suluhisho ni kulala na wanaume ambao watakulipa kwa huduma utakayowapa kisha waanzishe biashara na fedha zile.

Kwa kweli Huddah huwa haoni aibu kuzungumzia kazi yake.

Mwanamitindo mwingine ni Bridget Achieng ambaye pia aliongelea kuhusu tuhuma kuwa yeye hufanya biashara ya kuuza mwili wake. Ni bahati yake kwamba wanaume wanaovutiwa naye wana pesa. Kwa kweli, wafuasi wake hawakumwamini lakini alihakikisha kuwa wameelewa.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments