Huzuni baada ya baba wa watoto watatu kujitia kitanzi, Kinangop

Mwanaume mwenye umri wa miaka, 43 na baba wa watoto watatu kutoka kijiji cha Weru, Kinangop, kaunti ya Nyandarua alijitia kitanzi siku ya Jumapili.

Mwili wa Joseph Gakobo ulipatikana ukining'inia kutoka kwa paa la nyumba ya kuhifadhi vitu na mkewe Juamapili jioni. Alijitia kitanzi huku akitumia kamba.

Chifu msaidizi wa eneo hilo, Mary Njaure alisema bado haijabainika mbona Gakobo aliamua kujitia kitanzi kwani hata hakuwacha barua kabla ya kutekeleza kitendo hicho.

Alisema familia yake ilimuacha nyumbani walipoenda kanisani Jumapili asubuhi lakini hawakumpata waliporudi jioni. Mida ya saa tisa mkewe aliende kufungua chumba cha kuku na hapo ndipo alipouona mwili wa mumewe ukining'inia.

Njaure alilaani kitendo hicho akisema hakioneshi picha njema kwa watoto na jami kwa jumla . Aliwahimiza wakazi kujitokeza na kuzungumza kila wakati wanakumbwa na matatizo ili wasaidike badala ya kujitia kitanzi.

Majirani walioshtushwa na kisa hicho walimtaja bwana Gakobo kama jamaa mwenye bidii wakisema hawaamini kuwa alijitia kitanzi.

-Ndichu Wainaina