Huzuni Baada Ya Mwanamme Kufariki Baada Ya Kuchomwa Na Mkewe (AUDIO)

Hatimaye mwanamume kwa jina Franco Wesuswa kutoka kijiji cha Ngwelo eneo bunge la Webuye magharibi aliyedaiwa kuchomwa na mkewe mwezi jana ameaga dunia.

Kulingana na nduguye Mwendazake Moses Wafula ni kuwa Wesuswa aliungua asilimia sabini kufuatia majeraha ya moto yaliyosababishwa na mkewe kwa jina Maureen Wanyonyi aliyemumwagia maji moto.

Licha ya hayo yote Familia ya mwenda zake ikiongozwa na mwenyekiti wa ukoo huo, Protus Nyongesa imesema kuwa imemsamehe mshukiwa aliyeachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja na mahakama wakisema atalazimika kuwajibikia malezi ya wanawe.

Hata hivyo wakaazi wa  eneo hilo wakiongozwa na Patrick Nasongo na Mary Mukite wamekashifu kisa hicho na kutaka hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya mke huyo.

Skiza kanda ifuatayo.

&feature=youtu.be