Huzuni: Watu Saba Waaga Dunia Katika Ajali Karibu Na Mjini Voi

Watu 7 wameaga dunia baada ya gari aina ya matatu walimokuwa wakisafiria kugongana ana kwa ana na trela katika eneo la Ndara karibu na Voi barabara kuu ya Mombasa-Nairobi.
 
Walioshuhudia ajali hiyo wanasema matatu hiyo iliyokuwa imebeba kupita kiasi ilijaribu kupita magari mengine kabla ya kupata ajali.
Zaidi ya abiria 17 wamekimbizwa  kupokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi na Coast general wakiwa na majeraha mabaya.