IAAF kukataa ushindi wa Eliud Kipchoge, Ghost na Gidi watoa tamko

EGqdW2hX4AEZl_N__1571035590_51620
EGqdW2hX4AEZl_N__1571035590_51620

Gidi na Ghost wamekashifu kitendo cha IAAF kutoa taarifa kuwa ushindi wa Eliud Kipchoge hauwezi kutangazwa kama rekodi ya dunia ya mbio hizo.

Watangazaji hawa wamehoji kuwa liwalo na liwe Eliud ashaandikisha rekodi kubwa.

"IAAF wakubali au wakatae ushindi ushawekwa tayari..." Alisema ghost

Tamko hili linajiri baada ya Eliud Kipchoge kutwaa ushindi mkubwa katika mbio za Marathon mjini Vienna, Austria.

Kwa mujibu wa IAAF , ili mashindano yafikie sheria na kutambulika kama rekodi ya dunia,

Kuna masharti yanapaswa kufuatwa,

Mashindano lazima yawe yameandaliwa na shirika la riadha duniani IAAF ama shirikisho la riadha la nchini ambapo riadha hizo zinaandaliwa.

Aidha, Wanariadha wanaodhibiti kasi hawawezi kuingia katika mbio hizo kwa zamu na kutoka.

Tatu, Lazima wanariadha wafanyiwe vipimo vya matumizi ya dawa za kusisimua mwili pamoja na vinywaji vinapaswa kutoka kwa vituo rasmi na sio kupewa mwanariadha na wasimamizi wake baadhi ya vijisababu vingine.

Mashindano ya Viena hayakuwa mashindano bali yalilenga kuwapa motisha mamilioni ya watu duniani.

Eliud aliweka wazi kuwa hakuna mipaka ya ufanisi kwa binadamu yeyote duniani

Katika mahojiano na vyombo vya habari , Kipchoge alisema kwamba mbio hizo za Vienna zililenga kuwapatia changamoto wanadamu katika maisha yao ya kila siku.

Pia aliwashutumu wakosoaji wake.

Ninakimbia kuweka historia , ili kuuza #NoHumanLimited na kuwapa motosha zaidi ya watu bilioni 3 .

Sio swala la fedha bali kubadilisha maisha ya watu”, alinukuliwa akisema.