ICC Yaruhusu AU Kujumuishwa Katika Kesi Ya Ruto

Bw. William Ruto na Bw. Joshua Arap Sang. | picha: thehaguetrials.co.ke

Mahakama ya ICC imeruhusu Muungano wa bara Afrika (AU) kujumuishwa katika kesi inayomkabili naibu wa rais William Ruto.

AU sasa itaweza kuwasilisha maombi yake kortini kama rafiki wa mahakama ili kupinga uamuzi wa kukubali kutumiwa kwa ushahidi ambao umekanwa na walioutoa hapo mbeleni.

Katika habari husika, sasa ni rasmi kwamba mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria atafika katika mahakama ya ICC kama shahidi wa upande wa utetezi katika kesi dhidi ya naibu wa rais na mwanahabari Joshua Arap Sang.

Mawakili wa upande wa utetezi jana walikutana na Kuria ambaye alizua madai kwamba ushahidi dhidi ya Ruto ulipangwa.