Idadi ya watu walioathirika nchini na virusi vya Corona yafikia watu 110

km
km
NA NICKSON TOSI

Kwa mara nyingine tena taifa la Kenya limesajili idadi kubwa ya watu walioathirika na virusi vya Corona na kufikia watu 110 baada ya watu 29 kupatikana na virusi hivyo.

Watu hao walipatikana baada ya serikali kufanyia vipimo watu 662.

Kufikia sasa wakenya 3 wamepoteza maisha yao baada ya waaathiriwa 2 kuaga dunia mapema hii Leo.

Miongoni mwa watu hao 29,28 ni wakenya na raia mmoja akiwa wa kigeni.

Mutahi vile vile amedhibitisha kuwa naibu gavana wa Kilifi Gedion Saburi amepata nafuu na anasubiri kufanyiwa vipimo vya mwisho na madaktari.

Wahudumu wa boda boda nchini wametakiwa kubeba mteja mmoja na ni sharti wavalia barakoa ili kuzuiya kusambaa kwa virusi hivyo.

Serikali imetangaza kuajiri maafisa afya takriban 5000,ili kusaidia serikali kukabilina na virusi hivyo.

Mutahi aidha amesema hospitali zote za rufaa nchini zimeruhusiwa kuendelea kuajiri matatibu wengine na kuongeza kuwa vifaa zaidi vikiwemo vitanda 1000 vimepelekwa katika hospitali za kaunti na baadhi ya shule za mabweni ambazo zimetengwa kama maeneo ya karantini.

Serikali imeweka mikakati ya kuajiri wafanyakazi wengine wa afya takriban 6000 iwapo ugonjwa huo utakapokuwa umebisha katika kaunti zingine za taifa .

Mutahi pia amewataka watu kutulia katika eneo moja ili kuzuiya idadi kubwa ya watu kuambukizana virusi vya Corona.

Pia serikali imezitisha hatua ya watu kusafiri kutoka Nairobi wakielekea vijijini kama  njia ya kujaribu kuzuiya watu wengi kutangamana na watu ambao wametoka katika maeneo yalioathirika na Corona.