Idara ya polisi yazindua mfumo wa kidijitali wa kurekodi visa

Digital-OB--696x522
Digital-OB--696x522
Idara ya polisi nchini sasa imezindua mfumo mpya kidijitali wa kurekodio visa almaarufu OB ambao utafanikisha utendekazi wao nchini kama njia hya kuboresha huduma kwa wote .

Mfumo huo sasa utawafanya wakenya kupokea nakala ya ripoti kupitia barua pepe .

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang'i amesema maafisa wa polisi watakuwa na miezi 18 pekee kufahamu namna mitambo hiyo inavyofanyakazi.

Matiang'i amesema kuwa serikali inapania kuboresha huduma za idara ya polisi nchini kwa kutupilia mbali mfumo wa analogi ambao ulikuwa unachukuwa muda mwingi.

Amesema hadithi za kila mara za kupotea kwa faili hazitakuwepo kwani mfumo huo unalengo kuziba mianya hiyo.

Matiang'i pia amehoji kuwa watakao kuwa wakiwasilisha malalamishi yao kupitia mfumo huo watakuwa wakilipa na kupewa risiti papo hapo.

Idara ya polisi imekuwa ya hivi karibuni kuzindua mfumo baada ya Jaji mkuu David Maraga kuongoza wafanyakazi katika idara ya mahakama nchini kuzindua mfumo ambao utawawezresha wakenya kuwasilisha kesi zao mitandaoni pasi na kufika katika mahakama mbali mbali nchini.

Kwa upande wake inspekta jenerali wa polisi Hillary Mutyambayi amesema mfumo huo utafunga mianya yoyote ya kujaribu kuhitilafiana na taarifa zitakozokuwa zinawasilishwa katika vituo tofauti vya polisi.