IEBC yatoa kauli baada ya ODM kutishia maandamano

unnamed (3)
unnamed (3)
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amewajibu wafuasi wa chama cha ODM baada ya kutishia maandamano.

Chebukati amesema kwamba ni wapiga kura 333 ambao wamesajiliwa upya wakati wa  zoezi la usajili wa wapiga Kura.

Tume imesema kuwa rejista mpya imewasilishwa kwa Afisa mkuu wa IEBC katika eneo bunge la Kibra kwa uhakiki kabla ya kuwekwa wazi kwa umma.

IEBC imetoa majibu hayo saa chache tu baada ya ODM kutishia maandamano kushuturisha IEBC kutoa orodha ya usajili wa wapiga kura wa eneo bunge la Kibra.

Chama cha ODM Jumanne ilidai kupewa usajili kamili wa wapiga kura katika eneo bunge  hilo la kibra ikiwa ni pamoja na wapiga kura wapya.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati Jumatano alisema wamepokea wapiga kura 377 mpya katika usajili unaoendelea  mwaka 2019.

Mnamo mwaka wa 2017, idadi ya wapiga kura wa Kibra ilikuwa 118,276. Huku idadi ya sasa ikiongeza hadi  wapiga kura 118,609.

"Tume tangu Jumanne imechapisha mabadiliko hayo kwa usajili wa wapiga kura wa Kibra ulioorodheshwa hapo juu katika ofisi ya Afisa mkuu wa eneobunge la Kibra kwa ukaguzi  na uhakiki zaidi wa siku saba," alisema.

"Baadaye rejista  itathibitishwa na itapatikana kwa umma na kwa  vyama vyote vya kisiasa ikiwa pamoja n chama cha ODM.

Chebukati aliuhakikishia umma kuwa usajili huo utakuwa tayari kwa wakati kabla ya Novemba 7 wakati uchaguzi mdogo utafanyika.

ODM ilitishia kufanya maandamano  ili kushurutisha IEBC iweke hadharani usajili kamili.

Chama hicho kilisema kinataka orodha kamili ya wapiga kura tangu 2017, pamoja na tarehe na vituo vya usajili.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumanne, Mkurugenzi wa Uchaguzi za ODM  ambaye pia ni  mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed alisema kutokuwa na nia ya IEBC kuweka wazi  orodha hiyo kunafanya chama hicho kiwe na shaka ya uchaguzi mkuu ujao.

Kiti cha Kibra kilichoachwa wazi baada ya kifo cha  aliyekuwa mbunge Ken Okoth,  kimevutia wagombea 24.