ALICE WAHOME

IG Mutyambai aagizwa kumrejeshea mbunge Alice Wahome walinzi

Ilikuwa ni afueni kwa mbunge wa Kandara Alice Wahome baada ya mahakama kuu siku ya Alhamisi kumuagiza Inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai kumrejeshea mbunge huyo walinzi wake.

 

Soma habari zaidi;

Hakuna wapiga kura waliokufa wataibuka,’Ujumbe wa Akombe huku akimuomboleza Msando

 

 

Jaji James Makau alisema kwamba Inspekta mkuu wa polisi na mwanasheria mkuu hawawezi kuruhusiwa kutumia njia za ubaguzi kumpokonya ulinzi Wahome kwa sababu ya hila.

Wakati Wahome aliwasilisha kesi hiyo mwezi Februari mwaka huu, alidai kwamba hatua ya kupokonywa walinzi ilikuwa njama ya serikali kumuangamiza.

Mutyambai

“Kuondolewa kwa walinzi wangu kunaniacha na kauli moja tu, kwamba maisha yangu yamo hatarini na serikali inapanga kuniumiza, kunijeruhi au kuniua kutumia idara za usalama au majangili,” alisema.

 

Kupitia wakili Stephen Gitonga, Wahome alisema kwamba hakufahamishwa sababu zilizopelekea kuondolewa kwa walinzi wake.

Soma habari zaidi;

POA yachunguza ukatili wa pilisi katika City Hall

 

Jaji Makau alisema kwamba ikiwa Inspekta mkuu wa polisi alikuwa na mamlaka ya kuondoa walinzi wa Wahome, basi angestahili pia kumjulisha makosa yake ili asikizwe kwanza.

Court-Gavel-Thumb
Court-Gavel-Thumb

Makau alitaja hatua ya Inspkta mkuu wa polisi kama kinyume na sheria na kumuonya dhidi ya kuwapokonya wabunge walinzi bila kufuata taratibu zilizowekwa.

Mutyambai na mwanasheria mkuu Kihara Kariuki walikuwa wamedai kuwa Wahome alikiuka kanuni za uchaguzi kwa kumdhulumu afisa wa uchaguzi aliyekuwa akifanya kazi yake na hivyo kuvuruga amani.

Soma habari zaidi;

Mudavadi amepitisha muda wake kama kiongozi wa ANC-Msajili wa vyama

Photo Credits: Hisani

Read More:

Comments

comments