Ilikuaje:Nilikuwamfanyakazi wa nyumba kabla niwe mcheshi-Smartjoker

Michael Akala almaarufu SmartJoker alikuwa katika kitengo cha ilikuaje na kueleza jinsi alianza safari yake ya ucheshi na changamoto alizopittia kabla ya kujulikana.
"Nilikuja eneo la Kibera ili nianze kutafuta riziki kwa maana wazazi wangu hawakuwa na uwezo wa kunisomesha katika chuo kikuu

Nilianza kufanya kazi ya kufyeka nyasi, kisha nikaandikwa kama yaya kwa muda wa miezi tisa ambapo watu walini singizia kwa tajiri wangu uwa nalewa

Lakini ilikuwa uongo ni maumbile yangu." Michael Aliongea.

Mcheshi huyo ambaye ni wa tano katika familia ya watoto kumi na wawili ambebarikiwa na mke na wasichana wawili.

Michael alisumulia safari yake kuwa katika kipindi cha Churchill.

"Nilijua churchill kupitia kwa mcheshi wa KBC Maghoha, mimi nu muimbaji,rapper na hata mshauri wa watu, wimbo ambao Stivo simple boy alioutoa wa 'vijana wacheni mihadarati' nilikuwa nmeutoa enzi zile." Alisema.

Alisema kuwa kutokuoneka kwake awali katika kipindi cha churchill hajatoka wala hajapotea kwa ubaya.

"Kwa sasa niko katika masomo nasomea utangazaji ili niweze kuwa mtangazaji, nilijua nina kipaji cha utangazaji tangu nikiwa mdogo

Watu wengi wanakosa kusoma endapo wanatambua wako na kipaji cha usanii, lakini ilibidi nisome ili niendeleze utangazji." Alioeleza.

Cha mno ni kuwa alipatana na mke wake katika hoteli alipokuwa mhudumu wa hoteli na wamekaa katika ndoa kwa muda wa miaka nne.

Mshahara wake wa kwanza aliweza kupata baada ya kurekodi wimbo wake wa kwanza .

"Nilikuwa na shillingi elfu tano, ulikuwa mshahara wangu nilipofutwa kazi, niliingia katika studio na nikarekodi wimb wangu wa kwanza." Alieleza.