Ilikuaje: Haikuwa rahisi kubali kifo cha mke wangu-Dan Sonko

Katika kitengo cha ilikuaje Dan Sonko na mpenzi wake Bwire Ndubi walitembelea studio zetu na kisha kueleza vile maisha yao yamekuwa.

Wapnzi hawa waili wote ni waigizaji wa filamu.

"Kifungua mimba wangu alizaliwa kupitia oparesheni na wa pili pia alizaliwa na operesheni lakini kwa bahati mbaya aliaga dunia kwa sababu alikuwa amepoteza damu nyingi

Alipotoka kuzaa alipelekwa katika chumba cha hali maututi, alihitaji damu ya hapo kwa papo, watu walijitokeza kwa wingi na watu sita tu ndio walichaguliwa

Baada ya muda mfupi daktari aliniita na kuniambia mke wangu ameaga, ni habari ambazo si kuzichukua kwa urahisi." Alieleza Dan.

Imekuwa miaka miwili na miezi tisa tangu alipompoteza mkewe wake.

"Katika kuwalea watoto wangu nmesaidiwa sana wazazi wangu." Alisema Dan.

Mpenzi wake Bwire alikuwa na haya ya kusema,

"Nilijuana na Dan katika sekta yetu ya sanaa, na mkewe alikuwa rafiki yangu, kuna watu tofauti humu nchini siewezi sema Dan aliendelea na maisha yake kwa haraka baada ya kumoteza mke wake

Si hisi kama nimemsaliti mkewe kwa maana wakati alikuwa uhai sikuwa na uhusiano wowote na Dan, na hata katika kazi yetu sijawahi muona kama anaweza kuwa mpeni wangu 

Kwa sababu tayari alikuwa na familia yake." Alieleza Bwire.

Dan alisema kuwa alitoa pete ya ndoa ili kuanzisha uhusiano wake na Bwire na kusema kuwa alimjuwa mpenzi wake kabla amjue mwendazake mkewe.

Wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa muda wa miezi tano.

"  Uhusiano wangu na watoto wa Dan uko sawa kwa maana kifungua mimba tulikuwa marafiki sana, Dan uwa anamkumbuka mkewe lakini uwa nampa himizo." Alisema Bwire.

Dan alisema kuwa ni yeye aliuliza Winfred kuhusiana na swala la kuwa na uhusiano swala ambalo alikiri lilichukuwa muda mrefu .

'Mimi ndio nilimsukuma kwa sana, na marafiki wengi ndio wamenivuta nyuma kwa ajili wanakukejeli ukitaka kuendelea na maisha yako." Alisema.