Ilikuaje: Wazazi wangu waliaga dunia kwa sababu ya ukimwi-Revival Manoha

IMG_0617(1)
IMG_0617(1)
Msanii wa nyimbo za injili Revival Manoha Madunga hii leo alijumuika nasi studioni katika kitengo cha ilikuaje na kutueleza jinsi wazazi wake waliaga dunia kwa ajili ya ugonjwa wa ukimwi.
" Mama yangu mzazi aliaga dunia mwaka wa,1992, baada ya mwaka mmoja baba yangu aliaga dunia na kisha tukatengana na ndugu

Nilelewa na shangazi yangu na dada yangu pia na ndugu yangu walilelewa na shangazi tofauti,tuliletwa pamoja na sherehe za mazishi na si kitu kingine." Alisimulia manoha.

Baada ya kidato cha nne alikuja Nairobi licha ya yake kutojua mtu yeyote mjini.

"Nilisafiri nikaenda kwa dadangu aliyekuwa anauza nyanya, alinipa shillingi mia nane, nikatumia mia sita kama nauli na kubaki na shillingi mia mbili

Nilienda kuishi kayole, nikalala kwa nyumba ambayo haikkuwa imemalizwa kujengwa, kesho yake niliamka nikapatana na mzee ambaye alinsikiza na kunipa kazi ya kukata mboga."Alisimulia Manoha.

Manoha alijiuzisha na kikundi cha dawa za kulevya na kuanza kuzitumia,

"Nilianza kutumia dawa za kulevya kwa muda sasa, nilikaa mtaani kwa muda mrefu na kuwa kijana wa mtaa yaani chokora

Mwaka wa 2017, nilihubiriwa na mmoja wahibiri humu nchini na kunieleza jinsi kuwa na yesu ni raha na nikaokoka." Alieleza Manoha.

Alipokuwa anauza dawa za kulevya pesa alizokuwa anapata alikuwa anaenda kutafuta makahaba ili ashiriki ngono na wao.

"Nilikuwa nikipata hata kama ni mia moja naenda kutafuta kahaba nalala na yeye, natamani nione nchi ambayo vijana hawatumii dawa za kulevya na nchi ambayo haina ugonjwa wa ukimwi

Kama hakungekuwa na ukimwi singewapoteza wazai wangu na kama hakungekuwa na dawa za kulevya ama ulevi baba yangu hangemletea mama yangu ugonjwa." Alisema.

Alisimulia jinsi alivyoharibu wasichana na watoto wa wenyewe kwa kuuza dawa za kulevya anajuta na kutaka kuwabadilisha.