Ilikuaje: mchoro wa Uhuru nilimpa kama zawadi-Collins Omondi

collo
collo
Collins Omondi Okello ni msanii ambaye jina lake limetambaa sana wiki hii baada ya kumchora Steve Harvey.

Ndani ya studio katika kipindi cha ilikuaje Okello, 30, alikuwa na haya ya kusema,

"Mchoro wangu wa kwanza ulikuwa wa rais Uhuru Kenyatta, baada ya kumchora na kisha kuweka katika mtandao wa kijamii rais mwenyewe alinipigia simu baada ya kuona mchoro huo, hii ni kwa sababu uliambiwa na watu wengi katika mtandao wa kijamii.

Niliamka na nikapata watu wengi walikuwa wamenipigia simu, nilipopigia rais alinialika katika ikulu na nikaenda kumtembelea

Niligundua nina talanta ya kuchora nikiwa na umri mdogo sana." Alieleza Collins.

Collins alisema kuwa amechora watu kadhaa ikiwemo mtangazaji Jeff Koinange ambaye alimuita na kumshukuru kwa uchoraji wake.

Baada ya mchoro wa Steve Harvey kuenea , Steve aliouona na kisha akamtumia ujumbe na kumwambia anataka wakutane kwa sababu ya mchoro huo.

"Niliambia marafiki wangu wasambaze picha hiyo katika mitandao ya kijamii, baada ya Steve kuona picha hiyo alinituia ujumbe.

Aliniambia niende nchini humo ili tukakutane, katika chuo kikuu nilisomea maswala ya kifedha, mchoro wa uhuru nilimpa kama zawadi lakini kuna watu walinishukuru." Alisema Collins.

Collins ana mke mmoja na kubarikiwa na  watoto wawili.