ILIKUAJE: Angel afunguka kuhusu hali yake ya congenital hydrocephalus

Mwanahabari wa BBC, Ann Ngugi pamoja na mwanawe, Angel mwenye umri wa miaka 15 ndio waliokuwa wageni wetu katika kitengo cha Ilikuaje ndani ya Bustani la Massawe.

Mwanawe Angel anajulikana na wengi tangia mamake ajitokeze miaka kadhaa iliyopita na kuzungumzia hali yake ya kiafya.

Angel ni mmoja wa watoto waliozaliwa na hali ijulikanayo kama congenital hydrocephalus. Hali ambayo mtoto anazaliwa na maji mengi ndani mwa ubongo wake.

Na maji hayo husababisha kichwa cha mtoto kufura na kulingana na takwimu, watoto wengi walio na hali hii huwa hawafikishi miaka mitano. Isitoshe kama ataweza kuishi basi atakuwa kiwete.

Alipoulizwa kama hali yake huwapea watoto wenza fursa ya kumsumbua, Angel alisema huwa hatilii maneno yao maanani, licha ya kuumizwa moyoni.

"Unajua ukifanyiwa kitu unahisi vibaya kama mtu kwani sita tabasamu mtu akinitendea jambo mbaya. Mara nyingi huwa sifanyi lolote kwani nikiweka mambo moyoni nitapata magonjwa ya kusombwa na mawazo." Alisema.

Kwa upande wake Ann Ngugi, alisema kuwa hali hii hutokea pale ambapo mama mja mzito anapokosa kula chakula chenye madini ya iron, jambo ambalo anasema yeye alitilia maanani ila haelewi mbona mwanawe aliathirika.

Daktari alisema kuwa watamfanyia upasuaji kwani kichwa chake kinakuwa kikubwa kila uchao na wakaniambia akiendelea hivo aidha atakuwa kipofu, atashindwa kuzungumza au pia atafariki.

Mamake Angel anakiri kuwa safari ya mwanawe ni miujiza tupu na ndio maana wanamuimbia mwenyezi mungu kwani watoto wengi huwa hawapitishi miaka mitano.

Angel pia alisema baadhi ya changamoto anazopitia ni kuhisi kama kichwa ni kizito, na pia yeye huanguka mara kwa mara anapocheza na wenzake.

Alisema.

Nikiandika lazima nilalie mkono ili niweze kuandika kwani mimi huhisi kichwa ni kizito na huwa siwezi cheza na watoto kwani mimi huanguka.