Ilikuaje: Arrow Bwoy aeleza changamoto alizopitia kama mtoto wa mke wa pili

Ali Yusuf almaarufu Arrow Bwoy ameweza kulelewa maeneo ya huruma kaunti ya Nairobi.

Aliweza kuanza mziki kupitia kikundi cha (cubic) mwaka wa 2012.

Baada ya muda usiokuwa mrefu alianza kutoa nyimbo zake 2015, huku akijulikana kwa wimbo wake wa (gidigidi go down).

Alielezea kuwa hakulipa pesa zozote alioimba na msanii Cecile kwa sababu alipenda nyimbo zake hasa wimbo wa (digidigi) ndipo aliweza kumtafuta ili waweze kuimba pamoja.

"Cecile alipokuja nchini mwaka jana alisikia wimbo wa digidigi ambao umeenea sana kisha akanitafuta, nikaweza kuimba wimbo nikimshirikisha, na sikulipa pesa kwa maana ni yeye alinitafuta," Alieleza zaidi Arrow.