Ilikuaje: Cashy aeleza kilichomfanya atengane na mume wake Khaligraph

Karimi Muriungi almaarufu Cashy ni miongoni mwa wanawake ambao wako katika sekta ya usanii, sekta ambayo si wanawake wote ambao wanaweza kuwa hapo.

Cashy ni rapper ambaye alijulikana baada ya kuimba nyimbo kadhaa na aliyekuwa mume wake Khaligraph Jones.

Waliweza kupatana na mume wake Khaligraph Jones akiwa katika sekta ya usanii kisha akaweza kumchumbia na kumuoa kwa miaka mitano.

Baada ya miaka mitano Cashy aliweza kupitia vurugu katika familia yake na kupigwa au kuchapwa na mume wake baada ya kuvumilia kisha kuamua kuwa ametosha kuchapwa.

"Nilivumilia sana na sikuwa naambia mtu yeyote kwa sababu nilikuwa najali Khaligraph na pia, yaani vile watu watamchukua na vile watamuona katika sekta ya usanii,

"Nilitoka katika ndoa hiyo kwa sababu kuna mambo ambayo hayakunipendeza licha ya kuchapwa na Khaligraph,"Alisimulia Cashy.

"Wasanii wengi waliponihimiza na kunitia moyo niliona kuna watu wengi wanapitia mambo magumu kuliko ambacho nilipitia,"Aliongeza Cashy.

Aliweza kuwahimiza wanawake ambao wanapitia jambo kama lake wasiweze kunyamaza bali waweze kuzungumza na mtu.

Aliweza kusema kuwa alikuwa anaogopa kuwaambia wazazi wake kwa maana yeye ndiye kifungua mimba katika familia yao na hakuna vile angeweza kumwambia baba yake alichokuwa anapitia.

Baada ya kuzungumza na wazazi wake kwa sasa anaweza kusimulia kilicho mpata kwa dada zake. Cashy aliweza kuendelea na maisha kisha kupata mtoto mmoja.

Alisema kuwa hivi karibuni ataweza kuolewa na kuacha yaliyopita nyuma.