ILIKUAJE: 'Condom King' afichua mbona anapenda kazi ya kusambaza Kondomu

condom.king
condom.king
Stanley Ngara anayetambulikana kama 'Condom King' ndiye aliyekuwa mgeni wetu katika kitengo cha Ilikuaje.

Ngara ambaye amekuwa akipeana kondomu katika jiji kuu mara kwa mara, anasema anaifurahia kazi ile kwani nia yake ni kupambana na usambazaji wa virusi vya Ukimwi.

Lakini je kwa nini anaipenda kazi ile?

"Nimepoteza marafiki wengi sana kufuatia ugonjwa wa Ukimwi na kwa kweli HIV iko na lazima tumenyane nayo kwa njia tofauti. " Alisema.

Nimekuwa nikifanya kazi na shirika moja kwa miaka 20 ambayo inafanya kazi na vijana, watu walemavu ambao hufanya kazi ya kuhakikisha wamekomesha usambazaji wa ugonjwa wa Ukimwi.

Stanley anasema kuwa yeye alikuwa anasambaza kondomu kuanzia tano na zaidi pia kulingana na idadi ambayo watu walihitaji.

Kondomu lazima iheshimiwe kwani inakinga mimba, virusi vya Ukimwi na magonjwa ya zinaa. Kisha tunaangalia kuna mpenzi ambaye hataki kupata mimba na zile dawa za kuzuia mimba zinamdhuru kwa hivyo heri atumie kondomu.

Maambukizi yapo kwa kina nani sana?

Sasa hivi, watu kati ya umri wa miaka 18-24 hapo ndipo virusi viko. Kwa mfano watoto wengi wamezaliwa na virusi na wengine hawajui na wanafanya mapenzi bila kujikinga.

La pili hakuna kazi na kuna wengine wanafanya kazi ya ngono kupitia sponsors. Hatuna uwezo wa kuzungumzia mambo ya condom kwani wengine hutumia mara kadhaa kisha wanawacha.

Alisema kuwa kwa siku watu 50 hadi 89 huambukizwa virusi vya Ukimwi jambo ambalo linavunja moyo sana haswa ikibainika kuwa watu hawaogopi.