Ilikuaje: Cyrus Ng'ang'a azungumzia ubunifu uliompa hadhi duniani kote

Mgeni katika kupindi cha leo cha Bustani La Massawe alikuwa jamaa mmoja Cyrus Ng'anga Kabiru, msanii wa kuunda vitu vya kisanaa kama sanamu, miwani na hata baiskeli kutumia vyombo mbalimbali.

Jamaa huyu mwenye umri wa miaka 33 ana talanta na ubunifu mufti sana.

Amini usiamini, kupitia ubunifu wake na sanaa yake, ameweza kuishi maisha aliyotamani kuishi akiwa mdogo.

''Sahii naishi maisha niliyotaka kuishi nikiwa mdogo. Nimeweza kuishi maisha mazuri, nina gari nzuri na hata nyumba nzuri lenye nimejenga mwenyewe.'' Cyrus alisema.

Zaidi ya hayo, Cyrus alisema kuwa, hajajulikana sana kwa sanaa yake kwa sababu nchini Kenya watu hawawezi nunua sanaa na bado hawajatafuta chakula cha kuweka mdomoni.

''Huku Kenya sijajulikana sana kwa sababu hakuna mtu anaweza kununua kazi yangu na bado hana chakula cha kula.'' Cyrus alisema.

Vilevile, Cyrus alifunguka na kusema kuwa amelelewa mtaa wa korokocho na kwa sasa amefungua shule kule thika ya kuwasaidia watoto kutoka korokocho na mitaa tofauti tofauti ili waweze kujiendeleza pia kisanaaa.

''Hawa watoto wakifail pia mimi nitakuwa nimefail.'' Kabiru alisema.

Licha ya hayo, Kabiru alisema kuwa hata kama hakuweza kupata alama nyingi shuleni, kwa sasa anajiweza maishani.

Vilevile aliwaambia watu wapende kazi wanayofanya na kujitolea mzima mzima kufanya kazi hiyo kwani huenda kazi hiyo ndiyo itakayo kusaidia kufika unapotaka kufika maishani.

''Mimi nawaambia msibague kazi. Kama kazi yako ni kuchoma mahindi fanya kazi hiyo vizuri inaeza kuwa utajiendeleza na kazi hiyo. Usijidharau.''Cyrus alisema.

Ama kwa hakika, yote yanawezekana na penye nia, pana njia.