Ilikuaje: Fatuma Gedi afunguka kuhusu kanda ya ngono aliyosingiziwa

fatuma gedi
fatuma gedi
Mwakilishi wa akina mama wa wajir Fatuma Gedi ndiye aliyekuwa  mgeni wetu katika kitengo cha Ilikuaje.

Gedi alitembelea studio zetu takriban wiki tatu tangu aliposhambuliwa na mbunge wa Wajir Mashariki Rashid Amin katika majengo ya bunge.

Kisa hicho kilifanyika katika eneo la kuegesha magari bungeni wakati Bi. Gedi alipokuwa na mwakilishi wa akina mama wa Homabay Gladys Wanga walipokuwa wakielekea mkutanoni aliposhambuliwa na Bwana Amin.

Bwana Amin alimshtumu Bi Gedi ambaye ni mwanachama wa kamati ya bajeti kwa kukosa kulitengea eneo bunge lake pesa wakati wa ziara ya hivi karibuni ya kamati hiyo katika kaunti ya Wajir .

Akizungumzia kisa hicho, Fatuma Gedi alisema,

Kisa hicho hakikuwa cha kufurahisha najua watu wengi haswa wamama waliumizwa na zile picha kwani kama kiongozi na kama mama ilikuwa jambo mbaya sana.

Tulikuwa na Wanga na tukakutana na yule mheshimwa na tukasalimiana, akaniuliza mbona sikumwekea fedha katika bajeti. 

Jimbo 'Constituency' lake lilikuwa limetengewa millioni 80 za hospitali na bado kulikuwa na zingine bilioni moja ambazo zilikuwa zimetoka kwa wafahili, kwa hivyo tukatengea majimbo mengine fedha.

Gedi anasema kuwa alipojaribu kumweleza mbunge huyo, alikumbwa na matusi na hata alipoamua kumnyamazia, bwana Amin alimshambulia na kumgonga mara mbili.

Mama huyo wa watoto watatu pia alizungumzia kisa ambacho alisingiziwa kuwa kwa kanda ya ngono iliyosambaa katika mitandao ya kijamii.

Alisema kuwa licha ya tuhuma hizo moyo wake ulikuwa umetulia kwani alijua kuwa sio yeye na isitoshe mumewe alijua kuwa sio yeye hata.

Ilikuwa uchungu sana kwani kwanza nashukuru mwenyezi mungu kwani ukiona mtu akipigwa vita anafanya kazi. Kama hupigwi vita, hupangiwi kuuliwa ujue huna maana.

Nimejua nimefuatilia tukashika wale watu walipewa pesa na kumbe ni siasa na watu hawataki kuona nikiendelea. 

Lakini je kilichomjia akilini alipo ona kanda ile ni kipi?

Wakati niliiona nikaona ule mwili nakarudia mara mbili. Yule mama ana tattoo na mimi ni muislamu na sina tattoo nikaona amepaka rangi kwa kucha zake na sisi huwa tunapaka hena.

Kisha nikaangalia nyonyo, yule yake alikuwa na kubwa sana jameni, nikaangalia ile tumbo nakaona hapana, nikaangalia shape nikaona yule hata hajabeba vizuri.

Isitoshe mwili wake ni mweusi, uso mweupe kisha amevaa nywele za kubandika.

Gedia anasema kuwa walimpata mwanamblogu aliye fanya kazi ya kuunganisha ile video na kumshtaki.

Nilichukua hatua na yule mwanablogu tulimshika na mahali ilitoka ni Amerika na sauti ni ya kisomali. Ni video tatu zilibandikwa na cha muhimu wanasiasa ndio walifanya ile kazi.

Gedi alimalizia kwa kusema,

Muoga ndio ananyamazishwa kwani kuna kitu wameona kwangu na mie sio wa kuogopa na sirudi nyuma.

&t=631s