Ilikuaje: Harrison Mumia asimulia mbona hamuamini mungu

Mgeni wake Massawe Japanni leo katika kitengo cha Ilikuaje, alikuwa ni bwana Harrison Mumia ambaye anajulikana kwa kutomuamini mungu na ambaye pia ni rais wa wasiomuamini mola.

Harrison alidai kuwa alilelewa katika famili inayomcha mungu lakini anakiri kuwa 'alifunguka macho' pindi alipojiunga na chuo kikuu.

Anasema kuwa mungu hayupo na kuwa ni mawazo tu ya binadamu, isitoshe anaamini kuwa kama wa Afrika twapaswa kuchambua bibilia kwani lina makosa chungu nzima.

Nililia familia ambayo baba na mama walikuwa wakristo  kabla ya kubadilika nilipofika chuo kikuu.

Kila anayenijua anafikiri kuwa nimerogwa ama kuna kitu kibaya nami lakini nataka kusema kuwa sisi atheists ni watu wako sawa. Sinywi pombe, situmii madawa na nina kazi lakini ikifika kwa mungu simuamini.

Mamangu aliniombea sana na hadi sasa bado huniombea na ile iko ni kuwa maombi hayafanyi kazi. Babangu pia aliniombea lakini mda ulifika na akanielewa. Alisema Harrison.

Harrison anasema kuwa kinyume na jinsi wengi wanavyoamini, wanaoamini mungu yuko ndio wamepotea huku akisisitiza wasiomuamini mungu ndio watakao okoa Kenya.

Harrison alifichua kuwa yeye na wenzake hukutana Jumamosi ya mwisho ya kila mwezi kuzungumzia maswala yanayowakumba. Alisema kuwa kuna mipango yao kuweka mikutano yao siku ya Jumapili ili iwe kama dini la tatu.

Atheists in Kenya ina wanachama 600 ambao wamejiandikisha lakini tuna wafuasi elfu kumi. Tunataka kuweka mikutano yetu siku ya jumapili kwani tunataka kuwapa wakenya chaguo. 

Cha kushangaza ni kuwa Harrison huskiza nyimbo za injili lakini zenye mdundo kama wa lingala. Licha ya kutomuamini mola anadai pia ana imani shetani pia hayupo.