Ilikuaje: Hellen Mtawali aeleza vile alipo wapoteza ndugu zake wawili

Scoopnest.com
Scoopnest.com
Hellen Mtawali ni mwanamke ambaye amepitia uchungu mwingi katika njia ya kupoteza ndugu zake wawili. Mtawali, ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Daystar ambapo anafunza mziki.

Siku funza tu mziki pia ni msanii wa nyimbo, shahada yake ni ya ualimu na ana uwezo wa kuzungumza lugha kumi na sita.

Lugha hizi ni; Swahili, Kiingereza, Kigiriama, Kizulu na kindevele katika nchi ya Afrika Kusini, Kitanzania, Kinyarwanda na lugha zingine nyingi.

Pia ameweza kuimba nyimbo zake kwa lugha tofauti licha ya kuwa mluo.

Hellen alizaliwa kwa familia ya watoto 6 yeye akiwa wa pili wasichana 4 na wavulana 2. Hata hivyo, aliweza kuwapoteza ndugu zake kwa njia tofauti na kuhuzunisha.

"Nilipoteza ndugu yangu wa kwanza kwa njia ambayo ni ya uchungu, kulikuwa na vikundi viwili tulipokuwa tunaishi, ndugu yangu alikuwa kama kiongozi wa kundi moja.

Siku moja alipigiwa simu akaambiwa kuna mmoja wao anauwawa na hii kundi ingine ndipo alienda kumuokoa kufika hapo, alikatwakatwa kila mahali na mapanga na kufa. Alisema Mtawali.

"Kitu ambacho kiliniuma sana walikuwa wakimuuwa wakichukua filamu, hapo ndipo nilijua kuna watu tofauti nchini.

Ndugu yangu wa pili alikufa katika njia tatanishi aliweza kuuwawa akiwa nyumbani kwake hadi waleo hatujawahi jua kilicho muuwa ndugu yangu."Aliongeza.

Mtawali ambaye alikuwa mkuu katika kipindi cha Tusker project fame, alifunga pingu za maisha mwaka wa 2018 na mumewe ambaye walipatana katika bendi ya muziki.

Ushauri kwa wasanii.

"Wasanii wa Kenya mnapaswa kuingia katika usanii si kwa sababu tu ya pesa lakini kwa sababu wanapenda mziki, nimeeweka pesa zangu zote kwa kufunza watu usanii na mziki."Alisema Hellen.

&feature=youtu.be