Ilikuaje: Jacinta asimulia jinsi alivyokuwa msagaji (Lesbian)

Jacinta ni mtumishi wa mungu ambaye alijipata akiwa msagaji baada ya mume wake kufariki na kupitia changamoto mingi na kufukuzwa katika shamba lake.

Msagaji huyo aliweza taka kuwa mtawa tangu utotoni mwake na aliweza penda kushirikiana na wanawake kwa sana na wala si wanaume.

"Niliweza taka kuwa sista sana, ndipo mtumishi mmoja wa kanisa la kikatoleki aliweza kuniingisha katika sekta hiyo kuwa sista,

"Baada ya muda tuliweza enda misheni na kisha mchungaji (father) aliweza  anza kunishika matiti kwa maana alikuwa ana taka uhusiano wa kimapenzi,

"Niliweza toroka tukiwa misheni na kisha nikarudi nyumbani kwa wazazi wangu kwa maana sikuwa nataka uhusiano wa ngono na mwanaume yeyote," Alisimulia Jacinta.

Baada ya kutoroka aliweza kulazimishwa kuolewa licha ya kuwa hana hisia zozote za mwanaume. Katika ndoa yake aliweza kupata watoto watatu.

Jacinta Nzilani Kilonzo alisema kuwa alikuwa anavutiwa na wanawake na wala si wanaume.

"Nikiwa katika ndoa sikuwa nataka mume wangu anikaribie ata kidogo, ata wakati wa kufanya ngono tulikuwa tunasumbuana sana ili niweze kubali," Jacinta Alizungumza.

Mnamo mwaka wa 2008 mume wake aliweza kufariki na katika mazishi hayo kulikuwa na mvutano wa familia washirika wa kanisa na marafiki.

"Wakati wa mazishi kulikuwa na mvutano, familia haikuwa inanitaka tena, washirika wangu vilevile na hata marafiki zangu,

"Washirika waliweza kutoka kwa kanisa langu kisha nikafunga. Baada ya mazishi nilirudi humu Nairobi nilikokuwa naishi na mume wangu,

"Tulichapwa nikachapwa na watu, ni jambo ambalo liliweza kufanya kijana wangu awe na shida ya kimawazi na kisha kuenda katika hospitali ya Mathare ya watu wasiokua na akili timamu," Jacinta alisema.

Jacinta Nzilani Kilonzo alisema kuwa aliweza kujitambua kuwa yeye ni msagaji vizuri akiwa na miaka 16, baada ya changamoto hizo zote aliweza kukaa kwa muda wa miaka 8 ili aweze kumpata mpenzi ambaye ni msagaji kama yeye.

"Niliweza kuwa naongea na wanawake sana na si wanaume kwa maana nikizungumza na wanaume watakuwa wakitaka mapenzi,

"Nilikaa kwa muda wa miaka nane ili nimpate mwanamke ambaye ana hisia kama zangu, kwanza nilieza kupata mwanamke ambaye alikuwa mjane,

"Tuliweza achana kwa maana hakua na hisia kama zangu, baada ya muda mfupi niliweza kumpata mpenzi wangu aliyekuwa na hisia kama zangu,

"Mpenzi wangu ni mchungaji pia katika kanisa, huwa tunabusu na kufanya mambo ambayo watu hufanya," Alieleza Jacinta.

Alisema kuwa kuwa na mapenzi na mwanamke mwenzake si dhambi, na wakikamilisha vile katiba inavyosema wataweza kuoana, mpenzi wake hajaweza kujitokeza.