Ilikuaje: Joyce asimulia vile aliolewa akiwa na miaka 11

joycenjoroge
joycenjoroge
Joyce Njoroge ni mjane ambaye aliolewa akiwa na miaka kumi na moja.

Mama yake aliweza kuolewa na kisha kurudi kwao kwa ajili ya mgogoro wa familia.

Aliporudi kwao aliweza kuwa na uja uzito wa Joyce. Mama yake aliweza kurudi katika ndoa na kisha Joyce kukataliwa kwa maana hakuwa mtoto wa damu ya mume wa mama yake.

"Mume wa mama yangu walipomkujia kwao, waliweza mpata na kitoto ambacho si cha familia hiyo na kisha kumuambia aweze niacha kule mama yangu ametoka,

"Niliweza kuwachwa na nyanya yangu na mama yangu kurudi kwa ndoa, sikuwa naonana na mama yangu kwa maana nilikuwa mtoto wa uchungu wake,

"Nilieza kuteswa na wajomba na shangazi wangu nikiwa na miaka kumi," Alisimulia Joyce.

Joyce aliamua kuenda kujiua ambapo aliweza kupelekwa na rafiki yake ili kuenda kujirusha kwa mto ili aweze kumaliza maisha yake.

"Nilisikia nimepituia mambo mengi na mimi nilikuwa mtoto ambaye nimekataliwa katika familia (rejected child), nikaweza kufikiria kujiua,

"Nilienda kwa mto bali sikuweza kujiua kwa maana niliweza kusaidiwa na kushikwa na askari wa jeshi ambaye nilimueleza mambo ambayo nilipitia,

"Alinichukua kisha akanipeleka kwao, na kisha akaenda kwa mwaka mmoja, mama yake aliniweza kunilea kwa mwaka mmoja,

"Joseph aliporudi aliamua kunioa nikiwa na miaka kumi na moja, na singeweza kukataa kwa maana nilikuwa sielewi mzuri maisha," Alieleza Joyce.

Baada ya muda usiokuwa mrefu aliweza kuwa na ujauzito wa kifungua mimba wake akiwa na miaka kumi na moja, baada ya mwaka mmoja aliweza kuzaa mapacha akiwa na miaka kumi na tatu kisha baada ya mwaka mwingine mmoja akiwa na miaka kumi na tano akajifungua kitinda mimba.

"Mama mkwe aliweza kunifunza jinsi ya kuwa mke na mama, niliweza kuharibika sehemu ya uzazi kwa maana nilijifungua nikiwa mdogo," Joyce alisema.

Joyce akiwa na miaka 22 mume wake aliweza kufariki kwa kupigwa risasi akiwa vitani.

"Mume wangu Joseph alienda vitani kisha akapigwa risasi kwenye kifua, aliweza kurudi nchini akiwa akiwa na majeraha ya risasi,

"Aliweza kufariki Januari, baada ya kufariki tuliweza kufukuzwa katika kampi kwa maana tulikuwa tunaishi huko," Joyce alizungumza.

Baada ya kufukuzwa katika kampi hiyo aliweza kusaidiwa na rafiki yake Joseph, ambapo baada ya miaka kadhaa aliweza anzisha kikundi cha kuwasaidia wanawake wajane na ambao  waume wao waliweza kufariki wakiwa katika sekta yeyote ya polisi.

(Forces networks Global).

"Nilianzisha kikundi hicho baada ya kuteseka kwa muda kwa maana mume wangu alikuwa ameandikisha mali yake iweze kuchukuliwa na ndugu yake," Aliongea Joyce.

Aliasema kuwa wanawake wengi wameweza kusaidika kupitia kikundi hicho.