Ilikuaje: Kigame afichua alivyokuwa kipofu na kuwa alimuoa rafiki ya mkewe

Reuben Kigame, 52, ni msanii wa nyimbo za injili ambaye anajulikana kwa talanta yake ingawa ni mmoja wapo wa wasanii vipofu.

Kigame alifichua kuwa alipoteza uwezo wake wa kuona alipokuwa akila chakula cha jioni.

Akizungumza na mtangazaji Massawe Japanni, alieleza kuwa miaka iliyopita alikuwa na kituo cha radio chenye alifunga ili aweze kujiendeleza kimasomo. Alisomea shahada ya uzamivu (PHD) ya research na writing.

"Nilikuwa kipofu tangu nikiwa na miaka mitatu, na nilizunguka sana nikitafuta shule spesheli kwa ajili ya hali yangu mpaka nchi za ng'ambo. Nilisomea masters ya utangazaji na nikaanza kutangaza tangu nikiwa na miaka 19.

Nilikuwa katika stesheni ya citizen na Hope, pia katika stesheni yangu licha ya kuwa mkubwa wa hiyo kampuni niliweza kufanya (country show) Jumapili jioni na kipindi cha asubuhi."Alisimulia Kigame.

Reuben ni baba wa watoto wanne, wasichana wa kwanza watatu ni watoto wa mke wake wa kwanza huku kijana akiwa alijaliwa na mke wa pili.

Mke wake wa kwanza, Mercy alifariki kupitia ajali ya barabarani mwaka wa 2006 na kuweza kuoa mke ambaye anaitwa Julie.

"Julie alikuwa rafiki wa mke wangu, msichana wangu wa kwanza aliolewa mwaka uliopita, msichana wa pili ni mwalimu wa muziki katika shule yangu inaitwa Kigame music industry Eldoret." Aliongezea Kigame.

Uhusiano wake na watoto ni mzuri, na pia Kigame alikuwa na hoteli aliyo ifunga, aliweza kuwa mwalimu wa shule ya upili ya St Mary kaunti ya Kiambu.

Alifunza somo la historia na somo la dini yaani (CRE).

Msanii huyo alizaliwa Bunyore na kulelewa Kisumu, lakini amekuja kugundua kuwa wananchi wana ukaguzi wa kikabila wanapofikia umri wa kuoa.

"Mke wangu wa kwanza alikuwa ametoka Kirinyaga na mimi ni mluya, mke wa pili ni mluya nilipoteza uwezo wa kuona nilipokuwa nakula chakula cha usiku." Alisema

Huku akiwashauri vilema na walio na shida za kimaumbile, aliwaomba kutolalamika kwa maana wakilalamika hawawezi kujisaidia na chochote.

Pia alisema kuwa aliokoka alipokuwa katika shule ya upili, pia aliweza kuwania kiti cha ugavana cha kaunti ya Vihiga.