Ilikuaje: Maafikio ya Man Kush Kimaisha yakiwemo changamoto mwanzoni

Katika wasaa waIlikuaje, kwenye kipindi cha  |BustanilaMassawe, Massawe alimhoji mchungaji Paul Kuria Waweru maarufu kama Man Kush mbaye ni mhubiri katika kanisa la Home of Glory Joy Ministry lililoko barabara ya Thika.

Man Kush ambaye ni maarufu kwa ucheshi wake mbali na kuwa mchungaji na mfanyabiashara, anasema kwamba mwanzo wake haukuwa rahisi na hakuwai amini kwamba maisha yake yangemwendea hivi.

Man Kush alipoulizwa iwapo watu wanamchukulia kwa umakinifu kuhusu mahubiri yake, alisema kwamba ana wafuasi wengi wanaokuja kila mara na hao wana imani naye.

"Do people take you seriously?," Massawe aliuliza.

Naye Man Kush alisema, "Huwa naona watu wakikujanga."

Alipoulizwa maoni yake kuhusu wahubiri wengine kama Pastor Ng'ang'a, Man Kush alisema kwamba hangependa kujadili maisha ya watu wengine.

Lakini msikilizaji aliyepiga simu alisema kwamba haoni tofauti kubwa kati ya Man Kush na Pastor Ng'ang'a.

Hata hivyo Man Kush hakuungama au kukataa madai hayo.

Iisitoshe alisema kwamba wazazi wanafaa wawe vilelezo kwa watoto wao na mabadiliko kamili huanza na sisi mwenyewe.

Anasema kwamba baba yake alikuwa mlevi kupindukia na kufanya maisha yake ya utotoni kuwa magumu sana.

"Ukitaka kuwa kielelezo kwa mtoto wako, anza na wewe," alisema. "Soma mambo mapya, kila mara ili uongeze maarifa," aliongeza.

Pia alisema kwamba amekuwa mwanamasumbwi katika miaka ya nyuma ila aliacha kwa kukosa hela za kutosha.

Man Kush alisema anajutia kutozaa watoto wengi, alisema kwamba alitaka angalau awe na watoto wanane lakini hakuwa na kazi ya maana ila kuchimba choo mitaani.

"Najutia kutozaa watoto wengi na huwa namwomba Mungu anisamehe kila mara, nilitaka watoto watatu lakini kazi yangu ya kuchimba choo haingeniruhusu kuwalea," alisema.

Alisema kwamba wakati moja alianza kwa kuimba sokoni na wimbo wake ukavutia umati.

"Nilikuwa naimba sokoni na watu wakaanza kuacha kazi zao na kuja kunisikiza, sikua naitisha sadaka," Man Kush alisema.

Kulingana na yeye baada ya majuma mawili alikosa siku moja kwenda kuimba na watu wakaanza kumtafuta. Na hivyo ndivyo alivyoanza kazi ya kuhubiri.

Licha ya kufanya mtihani wake wa CPE mwaka wa 1998, anasema alifeli sana na akapata alama 19 tu. Lakini alikuwa roho juu kuwa hakuwa mjinga kupata alama hiyo.

Tangu aoe mke wake zaidi ya miaka 30 iliyopita, anasema kwamba hajawaimpiga mkewe.

Aliwakosoa wanaume wanaowadhulumu wanawake wao kwenye ndoa.