Ilikuaje: Mama yangu aliniambia babangu mzazi ni mjomba wangu-Jackie

Katika kipindi cha ilikuaje muigizaji Jackie Matubia alieleza jinsi maisha yake yamekuwa tangu utotoni mwake, Jackie alifahamika sana kwa uigizaji wake katika kipindi cha tahidi high.

"Mama yangu aliolewa tena baada ya kuachana na baba yangu mzazi, katika utotoni mwangu nililelewa na watu tofauti kwa maana mama yangu alipo olewa hakuenda na mimi katika ndoa yake mpya

Hii ni kwa sababu alikuwa anataka watu wa familia hiyo wanikubali, wakati huo alikuwa ananiambia baba yangu mzazi ni mjomba wangu

Baadae nilikuja kujua ukweli ambapo nilimkasirikia mama yangu sana lakini mwishowe nikakuja kumsamehe."Alieleza Jackie.

Mwaka jana ndoa ya Jackie ilivunjika na alikuwa na haya ya kusema kuhusiana na ndoa yake.

"Nilipojua ndoa yako haiendi vyema nilienda kumwambia mama yangu cha kusema alisema historia isiweze kujirudia tena, kwa sababu alinizaa na kuachana na baba yangu

Vilevile nilijifungua na mapema mwaka jana ndoa yangu ikavunjika, tulikimbilia ndoa yetu kwa sababu hatukua na mtu yeyote wa kutupa ushauri." Alieleza.

Si hayo tu aliongeza na kusema,

"Baba ya mtoto wangu aliniomba msamaha kwa mara nyingi, kuachana na mume wangu kuliadhiri mtoto wangu kwa sababu alikuwa analia sana." Alizungumza.

Hapo awali kuna uvumi ambao ulienea sana katika mitandao wa kijamii kuwa Jackie na mume wake walitengana kwa maana wote wawili walitoka nje ya ndoa lakini alikana madai hayo.

" Ni uongo kuwa tulikuwa tunaenda nje ya ndoa, hakuna vile unaeza enda nje ya ndoa mkiwa mmetengana kwa hivo ulikuwa uongo

Kwa kweli nilipatana na mume wangu katika mtandao wa kijamii wa instagram, tukakuwa marafiki kisha wapenzi

Kwa mara ya kwanza aliniambia kuwa ni dereva wa matatu lakini nikampenda hivyo." Alizungumza Jackie.