IMG_7277

Ilikuaje: Mamangu alinipata akiwa mchanga – Moji short baba

Msanii mashuhuri wa nyimbo za injili, James Muhia almaarufu, Moji short baba amefichua kuwa mamake alimpata akiwa mdogo wa miaka 16.

Akizungumza katika mahojiano ya moja kwa moja katika kitengo cha Ilikuaje, Moji ambaye ni kifungua mimba alifichua kuwa kwa ajili ya umri wake, mamake mzazi alimpeleka kwa nyanyake ambaye alimlea.

Ilikuaje: Fatuma Gedi afunguka kuhusu kanda ya ngono aliyosingiziwa

Alisema kuwa nyanyake ambaye alikuwa na watoto nane, alimchukua kama mtoto wake katika familia ambayo alikuwa anapendwa sana.

Mamangu alinipata akiwa 16 na tulikuwa tunaishi Mai Mahiu, hapo akanirudisha kwa nyanyangu kwa ajili bado alikuwa mdogo na nyanyangu hangemfukuza.

Shosho yangu alikuwa na watoto 8 na mimi nikawa kama kifunga mimba wake aliyependwa sana. Alisema Moji.

Huko Mai Mahiu maisha hayakuwa rahisi kwani walikumbwa na shida kadhaa. Kuna siku mvua kubwa ilinyesha na ikabeba nyumba yao, isitoshe bado kuna siku ardhi ilipasuka na kuwaathiri.

Mashida hayo ndiyo yalipelekea familia yake kuhamia Nairobi.

Ilikuaje: Nilikuwa nafanya kazi ya kuuza matiti – Boniface Kimanyano

 

Nyumba yetu ilikuwa kwa mlima, kuna wakati nyumba wakati ilibebwa na mafuriko na kuna wakti ardhi ilipasuka. Hapo tukahamia Nairobi kwani tulikuwa na shamba jiji kuu.

Ili shosho atulishe sisi wote aliuza katika soko zote wakiwa pamoja na mamangu.

Mamake mzazi aliaga dunia mwaka wa 2013 pindi tu alipomaliza masomo yake ya chuo kikuu na kumuacha katika hali ngumu ya kimaisha.

Anasema licha ya kuwachiwa majukumu ya ndugu zake, kilichomuuma ni kuwa hakupata nafasi ya kumfanyia mamake lolote kama zawadi ya kumlea.

Ilikuaje: Hopekid reveals student in threesome scandal with DK Kwenye Beat was suicidal

Mama aliaga 2013 baada yangu kumaliza shule na ilikuwa ngumu kwa sababu watu wengi hutafuta pesa ili washughulikie mama zao na kwa hilo ilikuwa ngumu.

Mimi hushukuru mungu kwani kuna vitu zingine huwezi elewa. Hapo nilimkimbilia mungu na akaniondolea mzigo huo.

Hata hivyo, baada ya mamake kuaga dunia, nyanyake alikataa Moji aishi na ndugu zake na kujitolea kuwalea na isitoshe shughuli zake za usanii hazitampa mda wa kutosha na ndugu zake.

Je ana mpenzi?

Nina mpenzi lakini naogopa kumweka kwa mtandao, nimesoma na wenzangu na siwezi taka changamoto zangu ziathiri mpenzi wangu.

Nataka kumlinda na pia uhusiano wetu ambao tumekuwa pamoja kwa takriban mwaka mmoja.

 

Moji ana wimbo mpya uitwao, sitadanganya amabao amemshirikisha Daddy Owen.

 

 

Photo Credits: Cliffton Apwoka

Read More:

Comments

comments