Ilikuaje: Mimi sio deadbeat - Walter 'Nyambane' Mong'are

Aliyekuwa mcheshi katika kipindi kilichovuma sana cha redykyulas, Walter Mong'are al maarufu, Nyambane amethibitisha kuwa yeye sio deadbeat na kuwa huwachunga watoto wake.

Nyambane ambaye alitembelea kituo cha Radio Jambo, katika majojiano na Massawe Japanni, alikuwa ana jiibu swali kuhusu uhusiano wake na aliyekuwa mkewe wa pili, bi Linda Muthama.

Nyambane hakuta kujibu maswali kuhusu uhusiano wao wa zamani lakini hakusita kusema kuwa wawili hao walipata mtoto mmoja ambaye wanafanana kama shilingi kwa ya pili. Pia alisema kuwa yeye humjali mwanawe na anashughulikia majukumu yote.

Kuna kitu inaitwa past na everybody has a past either one they are proud of or not, kwa unyenyekevu ningependa kumpatia Linda nafasi aendelee na maisha yake, mimi pia niendelee na yangu.

Mwanangu ananifanana na ninafanya majukumu yangu kama baba mkamilifu.

Kwa sasa, Nyambane ni naibu mkurugenzi katika ofisi ya uongozi wa vijana katika ofisi ya rais Kenyatta.

Je ana kumbukumbu zipi kuhusu kipindi cha Redykyulas na wasanii wenzake?

Sasa mimi na John Kiarie twazungumza na level fulani, yeye ni mbunge wa Dagoretti, Tony anafanya kazi ya advertising na kwa hivyo sote tumekua.

Tunafuraha kuwa chenye tulifanya siku zile ndizo zimetufikisha kwenye tuko.

Some of these greatest moments you stamble on it like an accident and it was not planned. Tony alisema let's do something crazy, KJ awe comedy nami niwe musician and that's how it came to be.

Msanii huyo ambaye aliwahi fanya kazi ya utangazaji na Massawe Japanni, alisema kuwa ha miss kazi zile ila anahisi kuwa ana miss walio fanya kazi pamoja.

I miss the people I worked with I don't miss the jobs I had. Kwa mfano Massawe unakumbuka tulifanya nawe kazi QFM na nakumbuka tulikuwa na wakati mwema sana pamoja.