Ilikuaje: Msanii Neddy asema kuwa hawezi ungana na kundi la Wasafi

Katika kipindi chetu cha Bustani la Massawe na mtangazaji wetu stadi Bi Massawe Japanni, mwanamziki wa Bongo Fleva kutoka Tanzania alifunguka na kusema kuwa, hawezi ungana na kundi la WCB ata iwe ameitwa na kuombwa aunge kundi hilo.

Sababu yake ya kusema hivi ni kuwa, ametosheka na kiasi ambacho mashabiki wake wanampenda na pia uungwaji mkono wa mashabiki wake umemtosha.

Neddy ni msanii wa nyimbo za Bongo fleva na balozi mzuri wa Tanzania, Afrika Mashariki  na Afrika nzima kwa ujumla.

Zaidi ya hayo, Neddy si mwanamziki wa nyimbo za bongo pekee yake bali pia mziki wa Afro Pop na pia dansa gwiji.

Neddy alianza usanii wake mwaka wa 2012 na muziki wake umepepea zaidi nchini Tanzania.

Vile vile, Neddy alisema kuwa wasanii wa Tanzania kama Diamond, Ali kiba na Vannesa Mdee ni wasanii  ambao huwapa moyo wanamziki kama yeye na mara kwa mara wanapo waona wanamziki hawa wakipata tuzo, wanatamani sana kuwa kama wao.

''Wanamziki kama Diamond, Alikiba na Vannesa wanatuinspire sana.'' Neddy alisema.

Neddy ni  jamaa ambaye amekuzwa katika dini ya kiislamu.

Vilevile, Neddy ni mtoto wa tatu katika familia ya watoto sita na mama mmoja. Baba yake alifariki akiwa mchanga sana.

Licha ya hayo, Neddy alifunguka na kusema kuwa,kitu amabcho anaogopa sana maishani kama mwanamziki ni kurudi chini katika usanii wake.

Aidha, Neddy alisema kuwa kutumia mitandao ya kijamii ili kujulikana na mashabiki, si watu wote wanaopenda kitu hicho na akasisitiza na kusema kuwa, kiki yoyote inaweza kumsaidia mtu labda kwa njia hasi au chanya.

Mwisho kabisa, Neddy alitoa wosia wake kwa vijana ambao wanataka kuwa wasanii na kusema kuwa,

''Zile dakika zako tatu ambazo unatumia kuandika wimbo, kurekodi wimbo na kuwapatia watu waskize, zitumie vizuri kuhakikisha kuwa, wimbo huo umewafurahisha watu na si tu kuwafurahisha, bali pia kuzungumza mazuri na kuishi na watu vizuri.