Ilikuaje: Mume wangu alifariki dakika nne baada ya kunipigia simu-Sarafina DeMathew

Sarafina De Mathew ambaye ni mjane wa msanii wa nyimbo za kikuyu alichukuwa fursa yake na kuja studioni katika kitengo cha ilikuaje kuelezea  jinsi mume wake alikufa na changamoto ambazo alipitia kama mke wa kwanza.
"Kabla ya ajali John De Mathew mume wangu alikuwa amenipigia simu na kuniambia nimfungulie lango kuu ili angie

Baada ya kuongea na yeye, mtu alinipigia simu na kuniambia kuna habari ambayo amesikia kuhusu baba ya watoto wangu

Nilichukuwa simu yangu na kumpigia bali hakupokea simu yangu mara nane, nilianza kushtuka ndipo watu nisiowajua walinipigia simu na kuniambia rambirambi zao.

Kwa mara ya kwanza sikuamini habari hizo, ni habari ambazo zilinishtua sana." Aliongea Sarafina.

Alizidi na kueleza jinsi watu wengi walitaka jina la De Mathew iaribike siku ya mazishi.

"Kuna watu wengi walitaka jina la mwendazake mume wangu iaribike wakati wa matayarisho ya mazishi na pia siku hiyo ya mazishi yake

Walikuwa wanataka tukosane na mke mwenzangu lakini kwa sababu niliona mambo hayo kwa umbali na sikuweza kukosana naye." Alizungumza Sarafina.

Alisema kuwa msichana wake aliadhiriwa sana na kifo cha baba yake.

"Msichana wangu aliadhiriwa sana na kifo cha baba yake, kwa hakika mume wangu alikuwa amezoeana na mwanawe sana hata wangeenda kutembea na yeye ili kujifurahisha.

Kuna wakati dadazake uwa wananiambia kama siyuko msichana wangu uwa anaeka nyimbo za baba yake na kuanza kulia hadi leo

Mume wangu alikuwa ananiogopa sana kwa sababu alikuwa ananitambua naomba sana, hata akienda kazini alikuwa ananiambia nimuombee sana." Alisimulia.

Hayo tu nusu aliongeza na kusema,

"Alikuwa akikosa akirudi nyumbani na anipate nikiomba ananiomba msamaha."Alisema Sarafina.