FotoJet (1)-compressed

Ilikuaje:Teacher Wanjiku aeleza safari yake anapohitimisha miaka 10 ya uigizaji

Mwigizaji Caroline Wanjiku maarufu kama Teacher Wanjiku anasema kuwa anafurahia sana kutimiza ndoto yake anaposherehekea miaka 10 kwenye ulingo wa uigizaji na ujeshi.

Hata ingawa anasema kwamba maisha yake hayajakuwa rahisi, ila kile anachofurahia anapohitimu mwongo moja ni kuwa kielelezo kwa wengi.

Anasema kuwa anafurahia sana kuona kuwa jinsia ya kike imejitoza kwenye sanaa hii ya ucheshi kinyume na vile ilivyokuwa awali.

PICHA: Haya Ndio Maisha Magumu Yanayomngoja Jowie Huko Manyani

Kwa sasa kama kusherehekea ufanisi wake, ameandaa hafla ya kuwapongeza wote waliomshika mkono akiwemo Daniel Ndambuki maarufu kama Churchill.

Kuhusu jinsi anavyozungumza, anasema kwamba amezoea hivyo na imekuwa desturi. Licha ya kwamba ilikuwa ni mtindo wa kuigiza, kwa sasa umekuwa mfumo wake rasmi wa mazungumzo.

Teacher Wanjiku licha ya kuwa alifunga harusi mwaka mmoja uliopita anasema kuwa, ana watoto 3 kwa sasa, kulingana naye alianza Twa twa mapema.

“Niko na watoto wawili wa kike na mmoja wa kiume, nilianza twa twa mapema.” alisema.

Teacher Wanjiku anasema kuwa imekuwa vigumu sana kuwa mtangazaji wa redio na hana azma kwa kuwa kulingana naye”inalemaza ubinifu”.

Ijapokuwa hakujua kilichotokea hadi sasa, kile anachofahamu ni kuwa show yake ilifutiliwa mbali baada ya muda mfupi

“I am a successful comedian, tulianza na brand na sasa imeenea kote dunia, tumefika hadi Marekani na kutuzwa,” alisema.

Teacher Wanjiku ambaye aliolewa na Victor Ber ambaye ni maneja wake, anasema kwamba anafurahia familia yake na ushirikano ambao wamempa.

Na wito wake kwa wanaume ni kuwa wanaowajibika.

“Wanaume mchukue responsibility yenu,” alisema.

Google Yachapisha Orodha Ya Watu Maarufu Waliotafutwa Sana 2019

 

 

 

 

 

Photo Credits: Amon Maghanga

Read More:

Comments

comments