Ilikuaje: Naiboi asimulia safari yake ya usanii kisha kuwa msanii maarufu

Katika kipindi chako ukipendacho cha ilikuaje na mtangazaji umpendaye Massawe Japanni alikuwa na msanii ambaye ameimba nyimbo ambazo zimependwa na kutambaa nchini kote.

Michael almaarufu Naiboi ni mwanamziki ambaye ametamba sana nchini Kenya aliweza kuingia katika sekta ya usanii mwaka wa 2003, na kisha kufungua studio ya iitwayo Pacho records ya usanii ili kuwasaidia wanamziki kukuza usanii wao.

"Nilitambua kuwa nina talanta ya usanii nikiwa na miaka 7, ambapo babayangu aliweza kunisaidia kukuza talanta yangu, alikuwa ana safiri kwa sana,

"Siku moja alipotoka Ghana aliweza kuniambia kuwa nimekuwa nikiimba sana na hakuna kitu cha maana nimefanya na usanii wangu kwa hivyo aliniambia niache usanii na nikalia sana,"Alieleza Naiboi.

Msanii huyo hana mzazi wa kike kwa maana mama yake mzazi aliweza kufariki akiwa mtoto mdogo. Alieleza kuwa kuna nyimbo ambazo ameandikiwa na ambazo amejiandikia.

"Niliweza kuimba wimbo wangu wa Welle Welle ambao ulitambaa sana kwa mitandao nikimshirikisha msanii Timmy Tdat na 'daktari' mwaka wa 2014. Kwa sasa nafanya kazi na mwelekezi wangu ambaye tulishirikiana pamoja,

"Sedrick ambaye sasa ni mwelekezi wangu kwa sasa,  nimeoa mke mmoja na mtoto mmoja,"Aliongezea Naiboi.

Awali Msanii huyo alikuwa anafahamika kama Rapdamu kisha akabadalisha akaitwa Naiboi jina mbalo lina julikana kwa sana katika sekta ya usanii.

Alisema kuwa ameweza kufanya kazi na wasanii mbalimbali. Alianza kama mwelekezi wa Pacho records kisha akaweza kuenda katika sekta ya usanii na kisha kujulikana kwa sana.