Ilikuaje: Nilibaka wanawake wengi bila kutumia kinga - Chock Dee

Chock Dee
Chock Dee
Katika kitengo cha ilikuaje katika kipindi cha Bustani la Massawe, Chock Dee, aliweza kueleza jinsi alivyoingia katika uhuni katika umri mdogo.

Alianzia wizi wa vitu vidogo vidogo kama kuku, nafaka na vingineo hadi kufikia kiwango cha kutumia bunduki na kuendeleza wizi wa kimabavu.

Baada ya kuiba na kupelekwa gerezani anadokeza kwamba hakuweza kujipata katika mateso kama kulawitiwa kwani alipata mzee aliyemsaidia sana “Nikiwa gerezani kuna mzee tulipatana gerezani tukakuwa marafiki na wakati mwingine kunicheka jinsi nilikuwa naiba vitu vidogo vidogo.”

Dee aliingia katika jiji la Nairobi mwaka wa 2001 ambapo aliishi na mamake, baadaye akatafuta jamaa fulani ambaye anasema alimkaribisha vizuri.

Alipohama kwa huyu jamaa aliweza kukodisha chumba chake na hapo anasema ndio alizama katika uhuni kabisa.“Kuishi pekee yangu sasa nikiwa huru na nikaendelea na bangi, pombe zaidi ya hapo nikaanza kujiunga na vikundi vya wizi”

Anaeleza kisa na ambapo aliibia muhindi na wakashikwa. “Tuliiba pesa ya muhindi elfu 100 na kupelekwa ndani, polisi akasema hatatuua wala hatatufunga jela ila tukaingia dili ya wizi na yeye. Wengi wa polisi wapo kwenye magenge ya wezi.”

Ameweza kufunguka jinsi alivyokuwa anawabaka wanawake “Niliwahi kubaka wanawake wengi bila kinga yoyote hadi sijui idadi yao.”

Alimalizia kwa kusema hawezi rudi katika tabia kama zile. Anasema kuishi maisha ya kujitafutia kuna amani zaidi