massawe japanni

Ilikuaje: Nilifanyiwe mke nikiwa miaka 16 – Kiambu MCA Mercy Nungari

Doh!

Mgeni aliyejiunga na Massawe Japanni studio anafahamika kama Mercy Nungari, nominated MCA wa Limuru East Ward Kiambu.

Ana fahamika kama Nungash kwa mafans. Anasema amepitia matatizo katika maisha yake. Safari moja alikuwa msichana wa kazi sasa hivi yeye ni MCA.

Amepitia mambo ambayo hawezi sahau. Anasema amezaliwa kwa umaskini watoto sita walikuwa wanalal wanaumwa na chawa na kunguni na alianza kufanya kazi akiwa mtot mdogo wa miaka tano.

Alisema’ Hapa nimefika ni mungu Sikuzaliwa hospitali, nilizaliwa kwa njia. Wazazi wangu walikuwa wanatoka kibarua Uchungu wa mtot ulikuja barabarani, Wazazi wangu walikuwa wachuna majani Ilikuwa inabidi saa zingine tunalala njaa’

Tulisoma kwa shida. tulilala chini mnaenda bila chakula, kunguni zimenikula zaidi.

Akisimulia stori yake katika kitengo cha Ilikuaje, Bi Mercy alisema

Ninafamilia lakini wakati unajua wakati watu wako na shida watu maskini, kuna wale watu waantake advantage. So kuna mwanaume alitook advantage of me na huyo mwanaume aliniambia ananipea kazi ya kuangalia watoto kwa nyumba yake, so it was something demonic kwasababu nilikuwa nafungiwa kwa nyumba 

Alifanyiwa nini?

Huyo mwanaume alinifanya bib yake, na nilikuwa napitia mateso unajua kwanza mimi nilikuwa mtoto so hata skuwa nataka kutoka juu ya ile kitendo alinifanyia sio kizuri na alikuwa na mabibi walikuwa wamekufa so nilikuwa naangalia watoto. Hata mama yake wakati walitafutwa na wanakijiji wetu, alisema mwenye ameona ni maid tuu. Na saa hiyo niko kwa nyumba Kuna hizi malwa za kufunga, huwezi ongea umefungiwa huwezi ongea na mpaka nikapelekwa nikafichwa mahali nikakaa kama mwezi sasa wazazi wangu wakatulia na sikuwa naweza kutoroka, tena huko sikuwa na chakula sasa huko ndio nilipata shida unaona nimeenda huko ndio mtihani form four.

Huyo mtu bado alikuwa anakuja na wanawake kwa nyumba sasa hatukuwa tunajua kitu, mimi nilikuwa nafanya kibarua kufulia watu manguo, napewa unga nipikie watoto wake. 

Alijikomboa aje katika maish na huyu mwanamume?

‘ah nikiwa mahali pale nilihubiriwa na nikaokoka. Mungu alinijia kupitia maombi, nilikuwa napitia magumu, nilibandikwa majina, na nikaamua kujiombea na kuenda kanisa ya PCEA, na kanisa ikanichukuwa na kutambua nilikuwa na talent ya uimbaji, na pia wao walikuwa wanajua hali yangu. Waliniambia tumekufungua, wakniambia wamenipa baraka yao, nilizidi kuvumilia kwasababu nilifikiria munug amenichagulia hiyo boma lakini huyo mtu wakashikana wakauza shamba na tukafukuzwa na auctioneers, sasa nikarudi kwetu. Walikuwa wanatuma brothers wangu wananiambia nitoke huko lakini sikuweza, hata nilikuwa napigwa brothers wangu wakiwa hapo.

 

 

Photo Credits: courtesy instagram/radiojambokenya

Read More:

Comments

comments